BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PERGAMON TZ LTD YAIPIGA JEKI TIMU YA SOKA YA MORO VETERAN SAFARI YA MWANZA.


Meneja wa kampuni ya Pergamon TZ Ltd Kanda ya Kati, Charles Mufikwa wa pili kutoka kulia akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Veteran Hamis Seleman kwa ajili ya ushiriki wa bonanza linalotarajiwa kufanyika jijini Mwanza makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa Morogoro Sekondari mkoani Morogoro, wa kwanza kulia ni Doglas Maele.
 
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya soka ya Moro Veteran FC imepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya sh 570,000 na kampuni ya Pergamon TZ Ltd kanda ya kati kwa ajili ya kushiriki michezo ya soka ya bonanza linalotarajiwa kufanyika April 26 hadi 28 Mwanza.

Bonanza hilo ambalo litawakutanisha wachezaji wa zamani waliowahi kutamba na klabu mbalimbali za soka hapa nchini zikiwemo Yanga, Simba, Pamba, Afrikan Sport, Reli na nyingine.



Akizungumza na wachezaji katika uwanja wa Morogoro Sekondari jana Meneja wa Kanda ya Kati kampuni ya Pergamon TZ Ltd, Charles Mufikwa alisema kuwa kampuni hiyo imetoa vifaa vya michezo seti mbili za jezi na mipira miwili vyenye thamani ya sh 570,000.

Mufikwa alisema kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya kampuni hiyo kuchangia shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo michezo na kijamii ambapo wametoa seti mbili za jezi sh 420,000 na mipira miwili sh 150,000.

Naye Msemaji wa klabu hiyo ya Moro Veterena Nickson Mkilanya alisema kuwa katika michezo ya bonanza hilo wanatarajia kuwatumia wachezaji waliowahi kuwika na klabu za Yanga, Simba, Reli, Afrikan Sport na nyingine.

Mkilanya alisema kuwa wachezaji ambao wanatarajia kuonyesha makali katika bonanza hilo ni pamoja na Hemed Mussa aliyewahi kuzichezea Afrikan Sport, ya Tanga, Idrisa Ndunguru, Reli na Coastal Union, Hamis Mzee, Pamba ya Mwanza, Adam Seleman, Reli na Simba na Ally Jangalu (mwanangu) Coastal Union ya Tanga.

Wengine ni Ally Bushir Pamba ya Mwanza na kueleza kuwa katika msafara huo wanatarajia kuondoka na timu ya veteran ya Wanawake.

Mikoa ambayo imethibitisha kushiriki bonanza hilo ni pamoja na mkoa wa Arusha, Tanga, Morogoro na Mwanza yenyewe.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: