Kwa ufupi
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema
kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni
la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na
kupata majawabu stahiki.
http://www.mwananchi.co.tzWaziri wa Fedha wa Tanzania kwa sasa, Dk. William MgimwaWaziri wa fedha aliyemaliza muda wake, Mustafa Mkulo.WAKATI hali ya umaskini inaonekana kuendelea kuwasumbua Watanzania, hatua za dhati za kudhibiti mali za umma bado ni tatizo nchini, huku wananchi wakiongea wanavyojua juu ya sababu za Serikali kushindwa kuwachukulia hatua wanaotajwa kufanya ufisadi.
Wapo wananchi wanaofikiri kuwa huenda kuna vigogo
wanahusika na ufisadi ndio sababu wanashindwa kuchukua hatua maana kuna
msemo ‘mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenzake.
Aidha wapo wanaowaza kuwa huenda wapo vigogo wanaona fedha za wananchi zikiibwa hazina athari kwao kwa vile wanaendelea na maisha kama kawaida.
Aidha wapo wanaowaza kuwa huenda wapo vigogo wanaona fedha za wananchi zikiibwa hazina athari kwao kwa vile wanaendelea na maisha kama kawaida.
Wakati watu wanasema hayo, Serikali mara kadhaa
kupitia viongozi wake mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, imekuwa ikisisitiza kuwa inafanya liwezalo kuboresha maisha ya Watanzania na kupambana na wizi wa mali za umma.
CAG Ufisadi na viongozi
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 akionyesha kuwa kuna ufisadi wa kutisha katika akaunti ya Deni la Taifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 akionyesha kuwa kuna ufisadi wa kutisha katika akaunti ya Deni la Taifa.
Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 ukurasa wa 158
inaeleza “Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa
tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwapo kwa marekebisho ya deni ya Shilingi
619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya
kuridhisha”.
Katika Taarifa hiyo, CAG Deni la Taifa linazidi kukua, mwaka unaoishia Juni 2012 lilikua kwa asilimia 17 kutoka mwaka ulioishia Juni 2011.
Katika Taarifa hiyo, CAG Deni la Taifa linazidi kukua, mwaka unaoishia Juni 2012 lilikua kwa asilimia 17 kutoka mwaka ulioishia Juni 2011.
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe anasema
kukosekana maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni
la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na
kupata majawabu stahiki.
Mikopo zaidi yaja
Bajeti inaonyesha Serikali itakopa shilingi takribani trillioni tano katika mwaka huu wa fedha.
Pia katika wakati huo, Serikali itapata shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanabainisha kuwa
ni dhahiri sehemu ya mikopo ambayo Serikali inachukua sasa itakwenda
katika matumizi ya kawaida.
Umaskini Tanzania, utajiri wa Malaysia
Wakati tunapata uhuru, tafiti zinaonyesha hapakuwa na tofauti kubwa hali ya uchumi wa Tanzania na nchi zingine kama Malaysia ambayo kwa sasa ni kati ya nchi za kuigwa Asia kwa uchumi imara.
Wakati tunapata uhuru, tafiti zinaonyesha hapakuwa na tofauti kubwa hali ya uchumi wa Tanzania na nchi zingine kama Malaysia ambayo kwa sasa ni kati ya nchi za kuigwa Asia kwa uchumi imara.
Mafanikio baina ya nchi kiuchumi yanatofautiana
kwa sababu za tofauti ya aina za taasisi walizoweka kwenye nchi husika,
sheria, kanuni na taratibu zinazoathiri uchumi walizotunga na namna ya
motisha walizoweka kwa ajili ya watu wao.
Kulingana na Takwimu za Benki ya Dunia mwaka jana,
uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 6.5 hadi 7, kiasi ambacho
kinaonekana kidogo mno.
Umaskini unaonekana kuwa mkubwa hasa maeneo ya
vijijini na baadhi ya maeneo ya mijini hasa kwa wasio na kazi na wale
walio kwenye sekta isiyo rasmi, umaskini wao unaongezeka kwa kasi.
0 comments:
Post a Comment