Kwa ufupi
Ndoto ya Azam kuisogelea Yanga kileleni imeingia doa
jana baada ya kulazimishwa sare 2-2 na Simba iliyoundwa na wachezaji
chipukizi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
http://www.mwananchi.co.tz
NDOTO ya Azam kuisogelea Yanga kileleni imeingia doa jana baada
ya kulazimishwa sare 2-2 na Simba iliyoundwa na wachezaji chipukizi
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Simba walikuwa wa kwanza kupata
mabao yao mawili kupitia mshambuliaji wao Ramadhani Singano kabla ya
Azam kuamka na kusawazisha mabao kupitia penalti ya Kipre Tchetche na
bao lililofungwa na Humpfrey Mieno.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi 47, wakati
Yanga wakiwa kileleni na pointi 52, huku Simba wakibaki nafasi ya nne
na pointi zao 36 na kupoteza matumaini ya kuiwakilisha nchi katika
mashindano ya kimataifa mwakani.
Katika mechi ya jana, Azam
walianza mpira vizuri na kufanikiwa kufika langoni mwa Simba katika
dakika ya kwanza baada ya shuti la John Bocco kutoka pembeni kidogo ya
goli.
Simba walianza vizuri jibu mapigo baada
ya mpira wa kona iliyopigwa na Mrisho Ngassa kutua kichwani mwa Shomari
Kapombe, lakini kipa wa Azam, Mwadini Ally alikuwa makini kuokoa hatari
hiyo.
Chipukizi Singano aliwainua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 11 akimalizia kazi nzuri ya Ngassa.
Wakati Azam wakiwa hawaamini kinachotokea Singano
alifunga bao la pili katika dakika ya 18, baada ya Ngassa kumtoka beki
wa Azam, David Mwantika na kupitisha pasi nzuri kwa chipukizi huyo.
Beki wa Azam, Mwantika alionekana mzito na
kushindwa kwenda na kasi ya Ngassa na Singano waliomgeuza walivyotaka na
kuipa Simba mabao mawili ya haraka.
Baada ya bao hilo kocha wa Azam, Stewart Hall
alimtoa Luckson Kakolaki na kumwingiza Hamis Mcha katika dakika ya 20.
Winga huyo alitumia dakika nane tu kabla ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki Miraj Mdigo na mwamuzi Oden Mbaga kutoa penalti iliyofungwa na Kipre Tchetche.
Winga huyo alitumia dakika nane tu kabla ya kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki Miraj Mdigo na mwamuzi Oden Mbaga kutoa penalti iliyofungwa na Kipre Tchetche.
Kiungo wa kimataifa wa Kenya, Humpfrey Mieno
aliisawazishia Azam bao katika dakika ya 71 akiunganisha vizuri mpira wa
adhabu uliopigwa na Mcha baada ya Tchetche kufanyiwa madhambi na Said
Nasoro Cholo.
Katika mechi hiyo, mwamuzi Mbaga alimtoa katika benchi, Kocha Hall na kumtaka aende kukaa jukwaani baada ya kumbwatukia akipinga uamuzi wake.
0 comments:
Post a Comment