Marehemu
Bi Kidude alikuwa ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) baada ya kutunukiwa nishani ya Sanaa na Michezo na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(kulia) katika sherehe za kutunuku Nishani katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam. Picha na
Ramadhan Othman, Ikulu.
Jina lake halisi ni Fatuma binti Baraka. Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu.
Muziki
huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya
muziki wa Kiafrikaumekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani
Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.Leo
hii ni Marehemu !.
Nguli na Mtunukiwa wa Nishani ya Uhuru wa
Tanganyika/Tanzania 2012, Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa
katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba
(7).
Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo
ni la kutumainiwa sana Zanzibar.
Bi Kidude aliwahi kusimulia
kuwa hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba
alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni
kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya.
Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.
Bi Kidude aliendelea kusema uimbaji
aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa
msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad.
Anasema
wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja
kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi
yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika
huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi
Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa
akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba.
Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.Alipokuwa
na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na
kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa.
Lakini
alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo
haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua
kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko
aling’ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma.
Lakini
ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako
aliendelea na shughuli zake uimbaji.
Bi Kidude hategemei kazi
moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya ‘wanja’ na ‘hina’
ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa
dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa ‘Unyago’ na
ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote
hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.
Watu wanasema ‘Utu uzima dawa’ Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu.
Lakini hakubakia hapo
alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude
anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake
Zanzibar.
Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.
Amekwisha pata tuzo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi
(ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX
ilienda kwake.
Nyimbo alizowahi kuimba ni
pamoja na Muhogo wa Jang’ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu.
Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.
Bi Kidude pia amekuwa
akishirikishwa na wasanii wengi wakongwe na chipukizi katika nyimbo zao.
Miongoni mwa nyimbo zinazotamba sana siku hizi ambazo Bi Kifude ameimba
na vijana wa kisasa ni za Msanii Ali Toll maarufu AT.
Mbali na AT lakini pia Bi
Kidude amewika na kung’ara zaidi katika wimbo mwingine wa vijana wa
Ahmada Umelewa wa Msanii Offside Trick ambao umepigwa marufuku kupigwa
kwa sasa visiwani Zanzibar.
MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI FATMA BINTI BARAKA AMINA
0 comments:
Post a Comment