BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 73 WENYE ULEMAVU WAUAWAWA KIKATILI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA SITA NCHINI TANZANIA.

Kwa ufupi

“Kinachotusikitisha ni kwamba pamoja na kasi hiyo ya mauaji, ni kesi nne tu ndizo zilisikilizwa mahakamani na kutolewa uamuzi. Sisi haturidhiki na kasi ya kusikiliza kesi za mauaji ya wenzetu wenye albinism,” alisema ofisa uhusiano wa shirika hilo Kondo Seif. 
http://www.freemedia.co.tz
WATU 73 wenye ulemavu wa ngozi (albino), wameuawa kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miaka sita iliyopita kuanzia mwaka 2007, Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Under the Same Sun (UTTS), limeeleza.

Shirika hilo lilitoa takwimu hizo jana jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka minne tangu kuanzishwa kwake. Under the Same Sun, ilianzishwa nchini mwaka 2008 na kusajiliwa rasmi Aprili 6 mwaka 2009.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa washirika hilo walisema kuwa mbali na mauaji hayo, watu wengine 34 wamejeruhiwa kwa kukatwa viungo mbalimbali vya miili yao, ikiwamo mikono na vidole, huku makaburi 19 yakifukuliwa kutafuta viungo vya wengine waliouawa na kuzikwa.


“Kinachotusikitisha ni kwamba pamoja na kasi hiyo ya mauaji, ni kesi nne tu ndizo zilisikilizwa mahakamani na kutolewa uamuzi. Sisi haturidhiki na kasi ya kusikiliza kesi za mauaji ya wenzetu wenye albinism,” alisema ofisa uhusiano wa shirika hilo Kondo Seif.


Kondo alisema Under the Same Sun imekuwa ikikutana na changamoto nyingi katika utendaji wake wa kazi ikiwamo jamii kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: