Kwa ufupi
Imesema kama nchi hiyo itakiuka, Serikali ya
Tanzania itaomba ushauri wa nini cha kufanya kutoka kwa jopo la
usuluhishi wa sakata hilo linaloundwa na marais wa zamani barani Afrika,
Festus Mogae (Botswana),Thabo Mbeki (Afrika Kusini) na Joachim Chissano
(Msumbiji) ambaye ndiye mwenyekiti. http://www.mwananchi.co.tzWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
DAR ES SALAAM.
BAADA ya Malawi kutangaza kujitoa katika mazungumzo ya mgogoro wa mpaka kati yake na Tanzania kwenye Ziwa Nyasa, Serikali imeitaka nchi hiyo kuacha kutapatapa na kamwe isithubutu kugusa eneo hilo la mpaka.
BAADA ya Malawi kutangaza kujitoa katika mazungumzo ya mgogoro wa mpaka kati yake na Tanzania kwenye Ziwa Nyasa, Serikali imeitaka nchi hiyo kuacha kutapatapa na kamwe isithubutu kugusa eneo hilo la mpaka.
Imesema kama nchi hiyo itakiuka, Serikali ya
Tanzania itaomba ushauri wa nini cha kufanya kutoka kwa jopo la
usuluhishi wa sakata hilo linaloundwa na marais wa zamani barani Afrika,
Festus Mogae (Botswana),Thabo Mbeki (Afrika Kusini) na Joachim Chissano
(Msumbiji) ambaye ndiye mwenyekiti.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema, “Nadhani
watasikia na kuelewa, Serikali ya Malawi iache kutapatapa, nchi zote
ilikoenda kulalamika kuhusu mgogoro huu, Tanzania tumekuwa tukielezwa na
hata hao wanaotueleza wanaishangaa sana Malawi.”
Kauli hiyo ya Serikali imekuja siku chache baada
ya Rais wa Malawi, Joyce Banda kusema kuwa mgogoro huo sasa utapelekwa
katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kwa madai kwamba juhudi za
usuluhishi wa kidiplomasia zimeshindikana.
Hata hivyo, uamuzi huo wa Malawi ni kinyume na
makubaliano baina ya nchi hizo mbili yaliyofanyika Novemba 7 mwaka jana,
jijini Dar es Salaam ambapo zilikubaliana kwamba jopo hilo ndiyo sehemu
ya mwisho ya makubaliano.
Katika maelezo yake, Rais Banda alisema nchi yake
imejitoa katika mazungumzo ya usuluhishi kwa madai ya kuhujumiwa na
Katibu wa jopo hilo ambaye ni Mtanzania, John Tesha kwa maelezo kuwa
anavujisha taarifa muhimu za Malawi kwa Tanzania kabla ya Tanzania
haijawasilisha taarifa zake kwa jopo hilo.
Akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mgogoro huo Membe
alisema hilo lilionekana na ndiyo maana ulitolewa uamuzi kwamba nafasi
ya Tesha itachukuliwa na Leonard Simao ambaye ni waziri wa zamani wa
Mambo ya Nje wa Msumbiji.
“Mwanzo walisema kuwa Tanzania tunataka kuwavamia,
tukatoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo, baadaye wakaibuka tena na kusema
kuwa tumetengeneza ramani ili kubadili eneo la mpaka, pia tulitoa
ufafanuzi kuwa ilikuwa mipaka ya nchi na sasa wamekuja na jambo jingine.
Novemba 17 mwaka jana tulikubaliana na hiki wanachokifanya Malawi ni
kinyume na makubaliano.
Ninawaomba waheshimu makubaliano yetu, hata kama jopo likitoa uamuzi wa kesi kupelekwa ICJ, Tanzania hatutakwenda mpaka tukutane na Malawi. Sasa kwa nini wao wanatapatapa?” alihoji Membe.
Ninawaomba waheshimu makubaliano yetu, hata kama jopo likitoa uamuzi wa kesi kupelekwa ICJ, Tanzania hatutakwenda mpaka tukutane na Malawi. Sasa kwa nini wao wanatapatapa?” alihoji Membe.
Alisema kuwa tangu kuibuka kwa mgogoro huo, Malawi
imekwenda kulalamika katika nchi za Uingereza, Marekani, Umoja wa
Afrika (AU) na katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC).
Huku akizungumza kwa ukali Membe alisema; “Wakati
tunasubiri jopo lifanye kazi yake tunaiomba Malawi isiguse eneo la mpaka
katika Ziwa Nyasa, na iwe hivyo hadi jopo au ICJ itakapotoa uamuzi.”
Mgogoro ulivyoanza.
Mgogoro huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi
bila kushauriana na Tanzania ilitoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni
kutafuta mafuta katika eneo la ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania.
0 comments:
Post a Comment