BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA SC KUENDELEA KUJICHIMBIA KILELENI LEO ?, INAKIPIGA NA OLJORO TAIFA LIGI KUU YA VODACOM.

Kwa ufupi
Vinara hao wa Ligi Kuu, wamewekeza pointi 49 kwenye msimamo baada ya kushuka dimbani mara 21, ikiiacha Azam FC katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46. 
http://www.mwananchi.co.tz/
DAR ES SALAAM. 
YANGA ina fursa nyingine kulisogelea karibu zaidi taji la ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, lakini hilo likiwezekana tu iwapo wataibuka na ushindi katika pambano lao dhidi ya JKT kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Vinara hao wa Ligi Kuu, wamewekeza pointi 49 kwenye msimamo baada ya kushuka dimbani mara 21, ikiiacha Azam FC katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 46.
Mahasimu wao na mabingwa watetezi, Simba wanachechemea kwenye nafasi ya nne wakiwa na pointi 34, ambapo wao watashuka dimbani kesho kuikabili Azam FC.
Kwa kuzingatia msimamo huo, Yanga ikifanikiwa kuizamisha Oljoro leo itafikisha pointi 52, ambazo zitaifanya isaliwe na deni la pointi saba pekee kabla ya kutawazwa mabingwa wapya.
Yanga yenye akiba ya michezo mitano mkononi, inahitahi ushindi katika mechi zake nne tu mfululizo ikiwamo ya leo dhidi ya Oljoro ili itwae ubingwa mapema.
Kama dhamira hiyo itafikiwa, basi wafikisha pointi 61 ambazo hazitaweza kufikia na timu nyingine kwenye ligi.
Pamoja yote ,mchezo huo hautakuwa rahisi kwa Yanga kwa vile Oljoro inayosifika kwa soka la nguvu, itaingia uwanjani kwa lengo la kulipa kisasi cha kufungwa mchezo wa kwanza.
Katika mchezo wa kwanza mwaka jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Maafande hao walizama kwa bao 1-0.
Oljoro yenye pointi 28 pia inahitaji ushindi utakaoipandisha juu kutoka kwenye nafasi ya nane inayoishikilia kwa sasa.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts amechekelea kurejea ‘vitani’ kwa mshambuliaji wake Jerryson Tegete, ambaye alikuwa nje ya dimba kwa takriban wiki mbili akiuguza jeraha la goti.
“Tupo tayari kwa mchezo na JKT Oljoro, taarifa nzuri kwetu ni kurejea kwa Jerryson Tegete aliyeungana nasi asubuhi kwenye mazoezini ya asubuhi baada ya kupona maumivu ya goti,” alisema Brandts.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: