
Wakati
taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba
kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za
kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na
majambazi karibu na eneo la kanisa hilo.
Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.
"Wakati
askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo
wamejitokeza kuwasaidia askari wetu.
Naomba unisaidie kukanusha siyo
kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema
Kamanda Kova hivi Punde.
0 comments:
Post a Comment