ika ya kwanza na sekunde 30.
Picha na JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
BONDIA Michael Mtambo wa klabu ya Mandera akiwa amedondoka chini baada ya kutandikwa konde na bondia Sudi Moto wa klabu ya DDC Boxing Club wakati wa pambano la utangulizi la raundi nne la uzani wa kg70 kwa KO dakika ya kwanza na sekunde 30.
Mwamuzi wa kimataifa wa ngumi nchini Emmanuel Mlundwa akimtangaza bondia Deo Njiku baada ya kumpiga mpiga Bingwa mtetezi, Omari Ramadhan wakati wa pambano la raundi 10 la kuwania ubingwa wa taifa wa PST la uzani wa kg 61 kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Deo Njiku alimtandika mpinzani wake kwa KO na kumnyang'anya mkanda huo usiku wa jumamosi.
Deo Njiku kulia akimtandika pinzani wake Omari Ramadhani raundi ya pili
Hapa Njiku kulia akimvizia Ramadhani kabla ya kumalizika kwa raundi ya pili ya pambano hilo. Bondia Mkuyu Katoto akijiandaa kumtwanga konde Pius Joseph wa klabu ya DDC Boxing ambapo mchezo huo Katoto kutoka klabu ya Mandera alishinda kwa pointi 40-36 katika pambano la uzani wa kg 63 la raundi nne.
Bondia Kudra Tamimu wa klabu ya DDC Boxing kulia akiajindaa kumsukumiza konde Daniel Kelly kutoka klabu ya Mandera kwenye pambano la raundi nne uzani wa kg 53, Kelly alishinda kwa pointi 38-37.
Hapa Super D akiwa na CD za kuona akiwa amezitandaza mkononi wakati akiwauzia mashabiki wa mchezo wa ngumi kwenye uwanja wa Jamhuri.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
BONDIA Deo Njiku wa Morogoro amefanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa wa PST baada ya kumtwanga bingwa mtetezi, Omary Ramadhani kwa K.O kutoka Dar es Salaam raundi ya pili wakati wa pambano la masumbwi la kuwania ubingwa huo uziti wa Kg 61 katika mchezo wa raundi 10 ambalo lilifanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jana usiku (juzi) mkoani Morogoro.
Katika mchezo huo Deo Njiku ndiye aliyeanza mchezo huo kwa kasi na kumshambulia mpinzani wake kwa kumtandika makonde mazito usoni na katika mbavu za tumbo huku Omary Ramadhi akitumia muda mwingi kujihami katika raundi ya kwanza.
Kuanza kwa raundi ya pili, bondia Omary Ramadhani aliendelea kujihami hali iliyompa nafasi mpinzani, Deo Njiku kuendelea kumshambulia kwa kumtwanga makonde mfululizo kwa kuendeleza kasi ya kurusha ngumi.
Baada ya kupigwa kwa kengele ya kuashiria kuanza raundi ya tatu bondia Omari Ramadhaman alimwita mwamuzi wa mchezo huo, Emmanuel Mlundwa na kumweleza asingeweza kuendelea na mchezo huo kutokana na kuumia katika mbavu na kufanya pambano hilo kumaliza katika raundi ya tatu kwa bondia Deo Njiku kushinda kwa kumtwanga mpinzani wake Omari Ramadhan kwa ushindi wa K.O na kutwaa ubingwa wa taifa wa PST.
Katika michezo ya utangulizi bondia Sudi Moto wa klabu ya DDC boxing alifanikiwa kumaliza pambano la raundi nne uzito wa Kg 70 kwa kumpiga kwa K.O Michael Mtambo klaby ya Mandera katika raundi ya kwanza kwa dakika 1 na sekunde 30 baada ya kumfulumishia makonde mazito mfululilo katika mchezo huo.
Wengine walioshinda katika michezo ya utangulizi kutoka klabu ya DDC boxing ni pamoja na Rahim Harid alimshinda Agogo Ramadhan wa klabu ya Mandela uzito wa Kg 68 kwa pointi 40-36, Mkuyu Katoto wa mandera akimshinda Pius Joseph katika pambano la Kg 63 kwa pointi 40-36 wakati Kudra Tamim wa klabu ya DDC boxing alipigwa na Daniel Kelly wa Mandera kwa pointi 38-37 na Twaha Kassim klabu ya DDC boxing akimshinda Gerald Kishoka wa klabu ya Mandera kwa pointi 48-35.
0 comments:
Post a Comment