http://www.mtanzania.co.tz
ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili mjini
Arusha jana asubuhi kwa ajili ya kuongeza nguvu za kuwasaka watu
waliohusika na mlipuko wa bomu katika Kanisa la Parokia ya Joseph
Mfanyakazi Olasite.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo waliwaambia
hayo wananchi eneo hilo jana jioni, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda
aliwatembelea kwa ajili ya kuwapa pole waumini wa kanisa hilo.
“Ndugu zangu, nawapa pole sana, Serikali yenu inakesha usiku na mchana,
napenda kuwaambia leo (jana) tumepokea askari wa FBI hapa kwetu wamekuja
kuongeza nguvu ya kuwasaka wahalifu hawa.
“Tunawaomba mwendelee
kutusaidia kwa kila aina na taarifa zenu tutazifanyia kazi muda wote,
tutahakikisha wote waliohusika wanatiwa mbaroni,” alisema Mulongo.
Kwa upande wake, Pinda alisema amesikitishwa na tukio hilo ambalo mpaka jana jio
ni limesababisha vifo vya watu watatu.
Alisema kwa wale wote ambao wamefariki, Serikali itagharamia mazishi yao kwa gharama na watazikwa kwa heshima zote zinazotakiwa.
“Nimemwagiza RC Mulongo, kuhakikisha wanafuatilia wale wote ambao wamefariki wanazikwa kwa gharama zote za serikali.
“Pia
nimemwagiza ahakikishe majeruhi wote wanaendelea kutibiwa kwa gharama
za Serikali na hata wale ambao wameruhusiwa kwenda majumbani mwao,
wafuatilie ili kujua wanaendeleaje,” alisema Pinda.
Alisema
taarifa alizonazo, ni kwamba majeruhi mmoja aliyekuwa akikimbizwa kwenda
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu alifia Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
“Majeruhiwa wengine 24, wameruhusiwa kwenda nyumbani na wengine wanaendelea na matibabu.”
Alisema
hadi jana jioni, polisi walikuwa bado wanamshikilia mtuhumiwa mmoja,
Victor Ambrose (20), ambaye anadaiwa kuwa alirusha bomu hilo.
“Mpaka
leo (jana), kuna Victor Ambrose anashikiliwa na polisi, nawashukuru
watu wote waliomfukuza na kumkamata baada tu ya tukio hili kutokea,”
alisema Pinda.
Alisema Serikali katika tukio hili, kamwe haitakwepesha ukweli na itatoa taarifa zote kwa wananchi.
Naye
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), aliwaambia waumini hao kuwa
Yesu alikufa msalabani na mwisho wa siku alifufuka na kushinda dhambi na
mauti.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment