BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LADY JAYDEE AKIPETA, LWAKATARE MAMBO MAGUMU, AREJESHWA MAHABUSU BAADA YA KUSIKILIZA KESI ZAO.

Mkurugezi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakare.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Jay Dee' akiwa na mumewe Gadner Hab
ash kabla ya wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa 3.

Belinda Msangula,Dar es Salaam
WAKATI kesi inayomkabili Msanii wa muziki wa kizazi kipya Judith Wabura, (Lady Jay Dee) akiahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu, Mkurugezi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakare amenyimwa dhamana kwa mara nyingine.

Lwakatare alipanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake, baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili na kumnyima dhamana.

Baada ya shitaka hilo kufutwa alibakiza kesi ya njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika.

Hata hivyo matumaini ya Lwakatare kupata dhamana ilitoweka na kurudishwa rumande hadi Juni 10 mwaka huu, Lwakatare amekosa dhamana hiyo baada ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo kuwa likizo.

Katika hatua nyingine kesi ya inayomkabili Lady Jay Dee iliahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu, Mwanadada huyo alifunguliwa mashtaka katika Mahamaka ya Hakimu Mkazi Kinondoni na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media
Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba. 

Chanzo http://www.habarimpya.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: