BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MMILIKI WA JAMIIFORUMS APATA AJALI NZEGA.

maxence-melo-ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi (kushoto) na Maxence Melo (mwenye koti) aliyepata ajali.
maxence-melo-ajali
HABARI na picha na AshaDii; at Jamii Forums.
 
MMOJA wa waanzilishi na wamiliki wa Jamii Forums, Maxence Melo, amepata ajali ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza kilometa chache kutoka Nzega mjini.

Mwanzilishi mwenzie na msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema Maxence na ndugu yake ambaye naye alikuwepo kwenye ajali hiyo, walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
 
Mushi alisema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana, haijaelezwa Maxence Melo ameumia kiasi gani ila taarifa zinasema kuwa ndugu yake amejeruhiwa vibaya .

Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: