Kwa ufupi
Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza walifunga kila
kipindi kwa Yanga na kutimiza utabiri wa muda mrefu, kwamba kikosi hicho
cha Jangwani kilikuwa bora kuliko kikosi cha Simba chenye mchanganyiko
wa vijana na wakongwe.
http://www.mwananchi.co.tzBaadhi ya wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kuifunga Simba
katika mechi ya kufunga msimu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam jana, Yanga ilishinda 2-0.picha na Emmanuel Herman.
DAR ES SALAAM, ARUSHA, TANGA.
DHAMIRA ya Yanga kusherehekea ubingwa wa Bara kwa kuifunga Simba ilitimia jana kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kuwanyoa mahasimu wao hao kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kufunga msimu ulioacha matukio ya aina yake kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
DHAMIRA ya Yanga kusherehekea ubingwa wa Bara kwa kuifunga Simba ilitimia jana kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kuwanyoa mahasimu wao hao kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kufunga msimu ulioacha matukio ya aina yake kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza walifunga kila
kipindi kwa Yanga na kutimiza utabiri wa muda mrefu, kwamba kikosi hicho
cha Jangwani kilikuwa bora kuli
ko kikosi cha Simba chenye mchanganyiko wa vijana na wakongwe.
ko kikosi cha Simba chenye mchanganyiko wa vijana na wakongwe.
Yanga iliyotwaa ubingwa kabla hata ya kumalizika
msimu, ilipania kushinda mchezo huo ili kunogesha sherehe za ubingwa wao
waliokabidhiwa jana na kitita cha Sh70 milioni kutoka kwa wadhamini,
Kampuni ya Simu ya Vodacom.
Kipigo hicho kinaiacha Simba katika nafasi ya tatu
ya msimamo wa ligi na kutwaa zawadi ya Sh25 milioni, ikimaliza msimu na
pointi 15 nyuma ya mahasimu wao Yanga iliyofikisha pointi 60 baada ya
ushindi wa jana.
Kabla ya mchezo huo wa jana uliovunja rekodi kwa kujaza mashabiki wengi, Yanga ilishuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0, Mei 5, 2012.
Kabla ya mchezo huo wa jana uliovunja rekodi kwa kujaza mashabiki wengi, Yanga ilishuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-0, Mei 5, 2012.
Katika mchezo huo, Simba itabidi wKiiza nusura
aipe uongozi Yanga dakika ya 21 baada ya kuunasa mpira uliochezwa vibaya
na beki wa Simba, Shomari Kapombe lakini akajikuta akipiga shuti ‘cha
mtoto’ kutokana na haraka zake, pia akikosa bao kwa shuti lake kutoka
nje dakika ya 35.
Mrisho Ngassa nusura afunge bao kwa Simba dakika
ya 51 kama siyo shuti lililotoka nje ya uwanja baada ya kutengenezewa
pande na Felix Sunzu, huku Simon Msuva wa Yanga akikosa bao dakika ya 56
baada ya mpira wake wa kichwa kutoka nje kidogo ya lango la Simba.
Kiungo wa Simba, Amri Kiemba naye aliendeleza
mlolongo wa kukosa mabao, kwani dakika ya 60 shuti lake ‘lililozaliwa’
na pasi ya Ngassa lilikosa shabaha lango la Yanga na kuruka juu.
Dakika ya 85 lilitokea tukio la kushangaza na
mpira kusimama kwa muda baada ya kiki kali ya adhabu ndogo ya Nizar
kuchezwa na Kaseja na mpira kugonga mwamba kabla ya kurudi na kumpiga
kichwani kipa huyo wa Simba na kulazimika kulala chini kwa muda.
Aidha, dakika ya 90 mpira ulisimama kwa muda baada
ya mwamuzi, Martin Saanya wa Morogoro kupigwa ngumi kwa bahati mbaya na
kuchanika sehemu karibu na jicho na beki wa Simba, Cholo aliyekuwa
kwenye mzozo na mshambuliaji wa Yanga, Kavumbagu.
Vilevile, mashabiki wawili wa Yanga walilazimika
kupewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia kutokana na kuzidiwa na furaha
ya ushindi wa timu yao, huku Ngassa wa Simba anayeelezwa kurudi Yanga
msimu ujao, akivalishwa jezi ya Wanajangwani hao na kuzungushwa uwanjani
akiwa amebebwa na mashabiki.
Aidha, katika mechi hiyo, iliyojaza mashabiki
kiasi cha kuweka rekodi, ulinzi ulikuwa mkali kwani hakuna magari
yaliyoruhusiwa kupaki eneo la maegesho ya magari ndani ya uwanja huo
tofauti na inavyokuwa kwenye mechi zingine.
Sababu kubwa ya kuimarisha ulinzi imeelezwa kuwa
ni hofu ya matukio ya kigaidi kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba,
Ezekiel Kamwaga.
0 comments:
Post a Comment