UNGEBAHATIKA
kumuona mwanaume mmoja, mkazi wa Sharif Shamba, Ilala jijini Dar, Beda
Mloka ‘Baba Tony’ alivyokuwa ametapakaa damu chapachapa, lazima uulize
kulikoni ambapo jibu ni moja tu la kushangaza, kisa cha yote hayo ni
fumanizi, Risasi Mchanganyiko lina kisa cha kusikitisha.
HAHABRI
kamili ni kwamba mwanaume aliyetajwa kwa jina la Baba Asha alidai
kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba Tony akiwa gesti na mkewe (jina
linahifadhiwa), tayari kwa ‘kugagadua’ naye amri ya sita.
Tukio hilo
la aibu ya milenia lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya Pumzika
iliyopo maeneo ya Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada ya
kumtia mikononi ‘mwizi’ wake ambaye mbali na urafiki pia ni majirani,
ndipo akamchakaza sura vibaya na kumsababishia kuvuja damu chapachapa.
NI MCHEZO.
Habari za
kina zilidai kuwa mke wa Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara ukaingia
ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe akachukua
kilongalonga hicho na kuufungua ujumbe huo.
Ilidaiwa kuwa mume alitaharuki kukutana na ujumbe uliokuwa ukimtaka mkewe kwenda Pumzika Guest House kukutana na jamaa huyo.
Iliendelea kudaiwa kuwa Baba Asha hakuyaamini macho yake, akausoma tena
ule ujumbe na ndipo akagundua sms nyingine nyingi, vocha na fedha za
mtandao alizokuwa akitumiwa ‘mai waifu’ wake kutoka kwa Baba Tony.
Chanzo kilidadavua kuwa baada ya kugundua mchezo mzima, Baba Asha
akatulia na kumsubiri mkewe atoke bafuni ili kuliweka sawa suala hilo.
MKE HUYO
Ilifahamika
kuwa mke aliporudi kutoka kuoga, mume hakuonesha dalili zozote,
alichokifanya ni kumwita mkewe na kumwambia kuwa achague moja,
kufungasha kilicho chake, aondoke nyumbani kwake au amwekee jamaa mtego
anaswe ili ajue mke wa mtu ni sumu.
Jibu lilikuwa rahisi kwani alikubali kuweka mtego ili amnase mbaya wake ndipo atamsamehe.
ACHEZWA NA MACHALE
Ilifahamika
kuwa ilipita wiki moja kimyakimya kwani mara ya kwanza Baba Tony
alichezwa na machale, alipofika kwenye gesti hiyo na kumwona mtu
anayemfahamu, alimwambia yule mwanamke waahirishe.
RISASI MCHANGANYIKO LATONYWA
Baada ya
kupata uhakika kuwa kuna tukio, ndipo chanzo chetu kikalitonya Risasi
Mchanganyiko kuwahi eneo la tukio na kuwa ‘stendibai’.
Risasi Mchanganyiko:
Habari tunazo nyingi na nyingine zipo kwenye
uchunguzi, si unajua Oparesheni Fichua Maovu ipo kazini? Lakini kama una
ya kwako tupe tuifanyie kazi mara moja.
Chanzo: Kwa taarifa yenu hapa Pumzika Guest House, Ilala kuna fumanizi, jamaa anamfumania rafiki yake na mkewe.
Risasi Mchanganyiko: Zungumza taratibu, tunashukuru kwa taarifa, tupe dakika sifuri.
‘NGOMA’ ILIKUWA HIVI
Kweli, ndani ya dakika sifuri, gazeti hili lilikuwa limejaa tele, tayari kwa fumanizi ambapo ‘ngoma’ ilikuwa hivi.
MTITI MKUBWA.
Chumbani
mtiti ulikuwa mkubwa ambapo Baba Tony alikutwa kama alivyozaliwa huku
mke wa mtu akiwa bado hajavua na ndipo mtiti ukaanza.
Katika purukushani, Baba Asha alimpa kibano ‘mwizi’ wake hadi akamchana
usoni na kumng’oa meno ya mbele, jambo lililosababisha kutokwa na damu
nyingi.
ACHOMWA BISIBISI KWENYE MAKALIO
Kama hiyo
haitoshi, ili kuthibitisha kuwa mke wa mtu ni sumu, Baba Asha alimchoma
jamaa huyo bisibisi kwenye makalio hadi askari alipoingilia kati na
kumchukua mtuhumiwa kisha akamtoa nje.
0 comments:
Post a Comment