Shambulizi katika kanisa Katoliki la Arusha la sababisha taharuki
Polisi nchini Tanzania
inawashikilia watu wa nane kwa madai ya
kuhusika na mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki la Olasit
viungani mwa mji wa Arusha. Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi
mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa
Tanzania. Wakati mwandishi wa BBC Baruan.
Muhuza akuzungumza akiwa
hospitalini
mjini Arusha amesema idadi ya watu waliofari dunia kufuatia mlipuko huo
ni wawili na wala sio watatu kama ilivyoripotiwa hapo awali. Polisi
mjini Arusha vile vile wamethibitisha kuwa waliokufa wakati wa tukio
hilo la kigaidi ni wawili.
Kwa wakati huu polisi wanachunguza
ni kulipuzi aina gani kilitumika wakati wa shambulizi hilo. Lakini
Baruan Muhuza ambaye alitembelea eneo la tukio mbali na
majeruhi hakuna hasara kubwa iliyotokea mahali hapo pia sakafi na kuta
za kanisa hilo hazikuchimbika sana.
Kutoka Dar es Salaam Leornad Mubali anaongezea kuwa watu wawili sana
wamethibitishwa kufariki dunia katika mlipuko huo uliotokea majira ya
saa tano asubuhi katika kanisa katoliki la Olasit nje kidogo ya mji wa
Arusha nchini Tanzania na wengine kadhaa kujeruhiwa huku balozi wa papa
na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya uzinduzi wa parokia
mpya ya mtakatifu Yosefu mfanyakazi wakinusurika pia.
Kwa mjibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa
kanisa katoliki jimbo la Arusha mlipuko huo unapotokea walikuwa tayari
katika hatua ya kubariki maji kwaajili ya uzinduzi wa kanisa ulikuwa
ukiongozwa na balozi wa Papa Fransis.
Shambulizi la Arusha Hata hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda
mfupi baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali watu kati yao wamefariki
huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mount
Meru mjini Arrusha.
Shughuli zote kuhusiana na ibada hiyo zimesitishwa huku watalaalamu
wa milipuko na polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na mlipuko huo.
Bado hakuna taarifa zozote
kuhusiana na chanzo halisi cha bomu hilo
ama kundi lolote linalodaiwa kuhusika na utegaji wa bomu hilo.
Hili ni
shambulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japo kuwa mwaka
huu pia kulikuwa na mtukio ya mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani
Zanzibar ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia
kanisani.
0 comments:
Post a Comment