TIMU NANE ZATINGA NUSU FAINALI UMISSETA NGAZI YA MKOA MOROGORO.
Mchezaji wa basketiboli Morogoro Vijijini Prodes James akimtoka David Liombechi wa Kilombero huku Lucas Mhinda akiwa tayari kutoa msaada wakati wa mashind
ano ya michezo shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro ambapo mchezo huo Morogoro Vijijini ilishinda kwa vikapu 35-30 kwenye uwanja wa jamhuri.
Mchezaji wa basketiboli Morogoro Vijijini, Prodes James akiruka juu ili kuweza kufunga kikapu.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU nane za mchezo wa soka katika mashindano ya michezo shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kufanya vizuri katika michezo yao katika makundi, katika mashindano yanayoendelea kufanyika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Wenyeji wa mashindano hayo timu ya soka ya Manispaa ya Morogoro wavulana walitinga hatua hiyo kupitia tundu la sindano baada ya kufungwa bao 2-1 na kushinda mchezo mmoja ambapo mchezo dhidi ya timu ya Kilosa na Morogoro Vijijini uliomalizika kwa sare tasa ya 0-0 ndiyo uliotoa mwanya wa wao kusonga mbele baada ya kundi hilo timu ya Kilosa kuambulia pointi mmoja na kuzifanya Morogoro Vijijini kuwa na pointi nne ikifuatiwa na Manispaa iliyomaliza kwa kupata pointi tatu.
Morogoro Vijijini ndiyo inaongoza kundi B ikiwa na pointi nne wakati Manispaa ina pointi tatu huku kundi A likiongozwa na Kilombero yenye pointi sita ikifuatiwa na Mvomero pointi tatu.
Kwa upande wa soka wasichana Morogoro Vijijini ndiyo imetinga hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kupata pointi sita ikifuatiwa na Kilosa yenye pointi tatu katika kundi A wakati katika kundi B Kilombero imekusanya pointi sita ikifuatiwa na Ulanga huku Manispaa na Mvomero zikichezea vichapo na kushinda kusonga mbele.
Katika mchezo wa basketiboli na netiboli wenyewe inacheza kwa mfumo wa ligi huku katika netiboli Manispaa inakaribia kutwaa ubingwa huo ikiongoza kwa pointi sita na kuonmbea ilishinde mchezo wake wa mwisho wakati katika basketiboli Manispaa iko katika nafasi nzuri wa kutwaa ubingwa huo ikiwa inaongoza kwa pointi sita na kusaliwa na mchezo mmoja na endapo itashinda itatangazwa mabingwa.
Kwenye mchezo wa wavu timu zilizotinga nusu fainali ni Manispaa kwa kukusanya seti nne na Ulanga katika kundi A huku kundi B Kilombero nayo ikiwa na seti nne wakati Mvomero ikijikusanyia pointi tatu.
0 comments:
Post a Comment