BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USAJILI LIGI KUU MSIMU WA MWAKA 2013/2013: HAWA NDIYO WACHEZAJI WALIOPO SOKONI

MWANANCHI,MICHEZO.Juma Kaseja ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inakaribia kumalizika.

 

DAR ES SALAAM.

HEKAHEKA za usajili zimeanza kushika kasi na tayari baadhi ya wachezaji waliomaliza mikataba yao katika klabu mbalimbali wameanza kujiweka sokoni kwa ajili ya kushinikiza kuongezewa mikataba mipya.

Winga wa Azam, Uhuru Seleman
i mwishoni mwa wiki aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook akitaka wadau wamsaidie kutafuta timu ya kwenda kucheza msimu ujao.
Uhuru aliandika “Leo Mei 24 nimetimiza miezi sita tangu nilipotua Azam, naomba mnisaidie nienda wapi Coastal Union, Simba au Azam.”
Naye mshambuliaji wa Kagera Sugar, Themi Felix alisema mkataba wake umemalizika na kutoa nafasi kwa klabu ambazo zimevutiwa na kiwango chake ili zumsajili.
“Nimemaliza mkataba na Kagera. Kwa hiyo ninafikiri ni muda mwafaka kwa timu ambazo zilivutiwa na kiwango changu kunisajili,”alisema Felix.
Wakati huohuo, beki wa Azam FC, Said Mourad aliliambia Mwananchi kuwa mkataba wake unakaribia kumalizika na yuko tayari kujiunga na timu nyingine.
“Mkataba wangu na Azam unakaribia kumalizika. Kwa sasa imebakia miezi kadhaa kabla ya kufika kikomo. Kwa hiyo kama kuna timu inataka kunisajili ninakaribisha mazungumzo,” alisema beki huyo.
Pia, wachezaji wa Simba, Ngalema Paul na Abdallah Juma wameamua kukatisha mikataba yao ya kuitumikia klabu hiyo.
Ngalema alisema ameamua kusitisha mkataba huo kutokana na chuki zinazoendelea baina yake na viongozi wa klabu hivyo na ameona hawezi kuendelea kuitumikia klabu hiyo zaidi ya kuangalia ustaarabu mwingine.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’ire ‘Mzee Kinesi’ amethibitisha kupokea barua za wachezaji hao kusitisha mikataba yao ndani ya klabu ya Simba, ambapo Ngalema alikuwa amebakisha miaka miwili wakati Juma mkataba wake ukimalizika Desemba mwaka huu.
Wachezaji wengine ambao mikataba yao ipo mwishoni ni makipa Juma Kaseja wa Simba anayemaliza mkataba Desemba mwaka huu, Hussein Sharrif wa Mtibwa na Deogratius Munishi wa Azam FC.
Wengine ni beki Shomari Kapombe wa Simba anayemaliza mkabata Desemba mwaka huu, Pia Amri Kiemba, Juma Nyosso, Haruna Moshi, Ramadhani Chombo na Abdallah Juma mikataba yao ipo mwishoni. Kwa upande wa Yanga ni Hamis Kiiza.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

rashid bumarwa said...

Angalia title, ni kweli 2013/2013 au ni makosa ya uchapaji?