Jack
PentezelKwa mujibu wa chanzo chetu (tunaficha jina lake), mastaa hao wa
kike, mmoja ndiye ataibuka mshiriki kwa mw
aka huu ambapo atakaa ndani ya mjengo kuanzia Mei 26, 2013 ambapo shindano litaanza rasmi.
aka huu ambapo atakaa ndani ya mjengo kuanzia Mei 26, 2013 ambapo shindano litaanza rasmi.
Jack
Patrick“Mimi nawamegea tu kwamba kati ya Wema, Baby Madaha, Jack wa Chuz
na Jack Patrick mmoja wao anakwenda Big Brother mwaka huu.
Wema
sepetu“Halafu ninachojua mimi, mshiriki ameshatumiwa taarifa kutoka
Multi Choice, ila tatizo wale jamaa wanataka mtu msiri sana, mshiriki
hatakiwi kumwambia mtu mpaka siku atakapoondoka,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Jumamosi lilipiga kiguu hadi Ofisi za Multi Choice jijini Dar na kuulizia Mbongo anayekwenda, likakumbana na majibu haya:
Baby
Madaha“Sisi pia hatujui. Unajua ilivyo ni kwamba huwa tunatuma majina,
sifa na anuani za watu kama watano kule Sauzi, halafu wao wanaangalia
vigezo vyao, anayeshinda anataarifiwa kutoka kulekule bila sisi kujua,”
alisema mtumishi mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Risasi
Jumamosi juzi Alhamisi liliongea na Jack wa Chuz ambaye alisema aliwahi
kuombwa kushiriki shindano hilo kwa sababu ya ushombe wake lakini
hakuweka wazi kama alijaza fomu za maombi au la!
Aidha,
Baby Madaha alipoulizwa alikiri kujaza fomu za kukusudia kushiriki siku
za nyuma akiwa sambamba na Wema lakini akasema hajui nani kashinda
ingawa lazima mshiriki ameshapatikana kati yao.
“Nasikia
mshiriki anatakiwa kujijua wiki tatu au mbili kabla. Kwa hiyo atakuwa
tayari anajijua, inakuwa siri ya mtu, hakuna anayeweza kujitaja kwa
watu,” alisema Baby Madaha.
Simu ya
Jack Patrick haikuwa hewani siku hiyo huku watu wake wa karibu wakisema
yupo nje ya Bongo kibiashara zaidi. Simu ya Wema muda mwingi iliita bila
kupokelewa hadi mpigaji akachoka.
Kwa
upande wa wanaume, wanaotajwa kushiriki shindano hilo mwaka huu ni staa
wa sinema za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, nyota wa Bongo Fleva, Khaleed
Mohamed ‘TID’ na aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Clouds TV, Rommy Jones
ambaye ni ndugu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
0 comments:
Post a Comment