Kwa ufupi
Msimu uliopita, kwenye mechi ya mwisho ya
mahasimu hao ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilishinda
5-0, wakati huo ikiwa tayari imeshatwaa ubingwa wa Bara.
http://www.mwananchi.co.tzNANI MWENYE SHABAHA ?, DAKIKA 90 ATAJULIKANA.
DAR ES SALAAM.
UBABE ubabe tu. Usemi huu unaweza kutumika leo wakati miamba ya soka Tanzania, Simba na Yanga itakaposhuka dimbani kuumana katika pambano la kuhitimisha Ligi Kuu litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo baina ya mahasimu hao una sura tatu
tofauti, kwanza kila timu inahitaji kuvuna pointi tatu ili kulinda
heshima yake, kulipa kisasi na kuendeleza rekodi.
Yanga inasaka ushindi ili kunogesha ubingwa wake
wa Ligi Kuu msimu huu, pia kulipa kipigo cha mabao 5-0 ilichokipata
kutoka kwa Simba katika mechi ya Ligi Kuu iliyopig
wa kwenye uwanja huo Mei 5, 2012.
wa kwenye uwanja huo Mei 5, 2012.
Nao Wekundu wa Msimbazi, baada ya kupokonywa taji
na kuambulia nafasi ya tatu, sasa wana kiu ya kutaka kuboresha rekodi
yao ya kumtundika mpinzani wake Yanga mabao mengi zaidi katika mechi
mmoja.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts akizungumzia matarajio yake kuelekea mtanange huo alisema:
“Bila kuifunga Simba ubingwa hauwezi kunoga, ndiyo maana tumejidhatiti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri Jumamosi.”
Kwa upande wake Liewig alisema: “Tunajua Yanga ni
Bingwa, lakini sisi pia tuna mipango yetu kama Simba ambayo ni
kuhakikisha tunashinda mchezo wa mwisho na hilo nina uhakika
litafanikiwa.”
Ubora wa vikosi:
Yanga itaingia uwanjani ikijivunia kikosi chenye wachezaji wazoefu katika mechi za ligi, lakini Simba itawategemea chipukizi wake walioitakatisha vyema mzunguko wa pili wa ligi Kuu, hususan Haruna Chanongo na Rashid Ismail.

Kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima atakuwa
‘mpishi’ mkuu wa mabao ya Yanga kwenye kipute hicho, kama itakayokuwa
kwa Amri Kiemba wa Simba ambaye kiwango chake cha juu msimu huu
kimewaacha wengi midomo wazi.
Rekodi za jumla:
Yanga na Simba zimekutana mara 100 katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu, kati ya hizo Yanga ilishinda mara 37, Simba mara 32, huku mara 31 zikitoka sare.
Yanga na Simba zimekutana mara 100 katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu, kati ya hizo Yanga ilishinda mara 37, Simba mara 32, huku mara 31 zikitoka sare.
Zaidi ya hapo, Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara 23 wakati Simba imefanikiwa kunyakua taji hilo mara 18.
Vita nyingine kali leo ni kati ya maafande wa
Mgambo JKT watakaokwaana na African Lyon iliyokwishashuka daraja, wakati
Toto African itaikaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,
huku Polisi Morogoro ikipepetana na Coastal Union.
0 comments:
Post a Comment