Akipatiwa huduma ya kwanza. Mwanamuziki Elias Barnabas 'Barnaba' akiweka udongo katika kaburi la mama yake mzazi, Mariamu Arubeth.
Baada ya kuweka udongo Barnaba akaishiwa nguvu.
Barnaba akiwa kapoteza fahamu wakati wa mazishi ya mama yake.
Baada ya kuzinduka. Akipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Mwanamuziki Elias Barnabas 'Barnaba' jana alipoteza fahamu wakati wa mazishi ya mpendwa mama yake mzazi, marehemu Mariamu Arubeth katika makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam. Hali ya Barnaba ilibadilika baada ya kuweka udongo katika kaburi la mama yake ndipo alipopoteza fahamu na kupatiwa huduma ya kwanza kisha kupelekwa hospitali.
0 comments:
Post a Comment