Chris Brown, muda mfupi tu akiwa anakabiliana na tuhuma za
kumdhalilisha mtu katika moja ya kumbi za starehe mwishoni mwa wiki,
sasa mapya yamemuibukia msanii huyu ambapo sasa imefahamika kuwa
amefunguliwa mashtaka ya kusababisha ajali na kukimbia.
Hii ni kutoka tukio la mwezi uliopita ambapo msanii huyu aliripotiwa kusababisha ajali ndogo ya gari dhidi ya mwanamke ambaye kwa mujibu wa mashtaka, staa huyu alikataa kumpatia taarifa sahihi za leseni na bima yake.
Msanii huyu amesema kuwa kwa sasa tayari wanasheria wake wanalishughulikia swala hili ambalo ameliita uzushi mkubwa kutokana na gari la kwake na la mwanamke aliyemgonga kutopata madhara yoyote, na pia kutokana na msanii huyu kuonyesha kujali kuchukua muda wake na kuzungumza na adui yake.
0 comments:
Post a Comment