MATUKIO YA KISIASA.
MATAIFA makubwa yanayounga mkono waasi nchini Syria yameamua jana
Jumamosi kuwapatia waasi msaada wa haraka wa silaha ili
kuweza kupambana na majeshi ya serikali na kuwalinda raia wa nchi hiyo.
anon la Hizboullah kuacha kuunga mkono utawala wa rais Bashar al-Assad.
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Qatar na mwenyeji wa mkutano huo Sheikh Hamad bin Jassem al-Thani amesema kuwa mkutano huo wa mjini Doha wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa zile nchi zinazojitambulisha kama "marafiki wa Syria", wamechukua uamuzi wa siri juu ya hatua muafaka ili kubadilisha hali ya mambo katika vita hivyo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry
Taarifa ya pamoja imesema kuwa "kila nchi katika njia zake" itatoa ,
haraka vifaa vinavyohitajika, ili waasi waweze kupambana na mashambulizi
makali kutoka majeshi ya serikali pamoja na washirika wake na kuwalinda
watu wa Syria."Baadhi wana wasi wasi
Sheikh Hamad amesema kuwa nchi mbili kati ya 11 zinazoshiriki zimeeleza wasi wasi wao, huku wanadiploamasia wakisema nchi hizo ni Ujerumani na Italia.
Wanaoshiriki wengine ni pamoja na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, Misri, Ufaransa, Jordan , Saudi Arabia, Uturuki, Umoja wa Falme za kiarabu na Marekani.
Marekani na Qatar zimetoa wito wa kuongezwa misaada kufikisha mwisho kile ambacho waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alichosema kuwa ni hali ya kutokuwa na uwiano katika medani ya vita.
Kerry amesema Marekani inaendelea kuhimiza mpango wa amani ambao unajumuisha kufanyika mkutano mjini Geneva pamoja na kuundwa kwa serikali ya mpito itakayochaguliwa na upande wa Assad na upinzani.
Mapambano mjini Damascus.
Lakini ameongeza kuwa waasi wanahitaji msaada zaidi ili kuweza kufika Geneva na kuweza kuweka hali ya uwiano katika vita.
Sheikh Hamad amerudia matamshi ya Kerry , akisema kuwa suluhisho la amani , haliwezi kufikiwa hadi pale uwiano katika vita utakapofikiwa, ili kuweza kuulazimisha utawala wa Syria kukaa pamoja na upinzani katika mazungumzo.
Siku ya Alhamis , jeshi la Syria huru limesema kuwa linahitaji silaha za kupambana na ndege za kivita pamoja na vifaru.
Mwanadiplomasia wa mataifa ya magharibi mjini Doha amesema jana Jumamosi kuwa mkuu wa jeshi hilo la Syria huru , FSA jenerali Selim Idriss amewasilisha orodha ya maombi na kwamba orodha hiyo imekubaliwa kwa kiasi kikubwa.
"Kila mmoja atasaidia na kutoa msaada mzuri," mwanadiplomasia huyo amesema , na kuongeza kuwa msaada huo utakuwa muhimu na pia ni hatua muhimu ".
Rais Bashar al-Assad.
Wanamgambo wa Hezboullah na wapiganaji wa Kishia kutoka Iraq pia wamekuwa wakipigana katika eneo la eneo la ibada la Washia katika mji wa Sayyid Zainab kusini mwa mji mkuu Damascus, wakati makamanda wa kijeshi kutoka Iran wanaaminika kuwa wanatoa ushauri kwa maafisa wa jeshi la Assad katika mashambulizi yao dhidi ya waasi.
Mawaziri hao wamesema kuwa kuongezeka kwa hali ya kivita ya kimadhehebu katika mzozo huo pamoja na kuingilia kati kwa wapiganaji kutoka nje, kunatishia umoja wa nchi ya Syria na kupanua mzozo huo katika eneo lote.
Pia wameeleza wasi wasi wao mkubwa kutokana na kuongezeka kwa makundi ya kigaidi pamoja na kuongezeka hali ya misimamo mikali ya kidini nchini Syria. CHANZO http://www.dw.de
0 comments:
Post a Comment