DODOMA/ DAR ES SALAAM.
HUKU mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ukiwa unahitimishwa leo, wabunge wa CCM wameshindwa kupata mwafaka wa kusimama pamoja ili kuipitisha.
HUKU mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ukiwa unahitimishwa leo, wabunge wa CCM wameshindwa kupata mwafaka wa kusimama pamoja ili kuipitisha.
Wabunge hao walikutana jana jioni kwenye Ukumbi wa
Pius Msekwa, Dodoma kujadili tofauti baina yao na kuwa na msimamo wa
pamoja, lakini mgawanyiko wa dhah
iri ulionekana ndani ya kikao hicho baadhi wakipinga huku wengine wakiunga mkono na kuwatisha wenzao.
iri ulionekana ndani ya kikao hicho baadhi wakipinga huku wengine wakiunga mkono na kuwatisha wenzao.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho
zinasema wabunge wengi wa chama hicho walipinga bajeti hiyo wakiitaka
Serikali kuzingatia mapendekezo ya marekebisho waliyoyatoa wakati
wakichangia mjadala. Mambo makubwa mawili yaliyowagawa wabunge hao ni
suala la kupandishwa kwa ushuru wa petroli na hatua ya Serikali
kupunguza asilimia moja tu kwa kodi ya mshahara (PAYE).
Pia wabunge hao waliitaka Serikali itekeleze
mapendekezo ya marekebisho yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Katibu wa Wabunge wa
CCM, Jenister Mhagama alitumia muda mwingi kuwashawishi wabunge
kuikubali bajeti hiyo. Aliwaambia wabunge hao kuwa yeyote anayejiona
hawezi kuunga mkono bajeti hiyo ni bora asiingie kwenye kikao cha kesho
(leo).
Habari zaidi zinaeleza kuwa hoja hiyo iliungwa
mkono na Mbunge wa Sikonge, Tabora, Saidi Nkumba aliyesema anayepinga
bajeti hiyo, siyo tu asiingie katika kikao hicho, bali atafute chama
kingine.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy alisema mbunge wa CCM atakayepinga ongezeko la kodi ya mafuta leo halitakii mema taifa.
Bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk
William Mgimwa Juni 13, mwaka huu ilipendekeza punguzo la asilimia moja
la kodi hiyo, huku mafuta yakiongezwa kodi kwa asilimia mbili kwa dizeli
na petroli asilimia moja.
Mbunge wa Geita, Dk Hamisi Kigwangalla ndiye pekee
aliyepinga waziwazi bajeti hiyo kwa upande wa CCM wakati wa mjadala
akisema haina jibu kwa suala la ajira kwa vijana, mfumuko wa bei, njaa,
uhakika wa chakula na afya. Pia alipinga ongezeko la kodi.
Licha ya kuunga mkono bajeti hiyo, wabunge wengine
wa CCM waliikosoa wakibainisha kasoro kadhaa. Mbunge wa Kigoma Mjini,
Peter Serukamba alisema inawapa mzigo wafanyakazi kwa kuwapunguzia PAYE
kidogo wakati kwenye simu, mafuta (petroli na dizeli), vinywaji vyote
kodi imeongezwa.
Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina na Kangi Lugola wa
Mwibara kwa nyakati tofauti, waliikosoa wakisema inamkandamiza
Mtanzania wa kawaida. Bajeti hiyo inayokadiriwa kufikia Sh18.2 trilioni
imeelekeza nguvu zaidi katika sekta za maji, nishati ya umeme,
miundombinu ya barabara, ujenzi wa bandari, reli, na elimu.
Bajeti ya mwaka huu haikujadiliwa na wabunge wa
Chadema kwani hawakuwapo kwa takriban wiki nzima. Pia hakikusoma bajeti
yake mbadala bungeni kutokana na wabunge wake kwenda Arusha baada ya
kutokea kwa mlipuko wa bomu Juni 15, kwenye Uwanja wa Soweto wakati wa
kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani na kusababisha vifo vya
watu wanne, kujeruhi zaidi ya 60.
CHANZO MWANANCHI.
CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment