Mdee amekuwa
akiendelea na mazoezi yak echini ya Mbunge wa CCM, Idd Azzan ambaye pia
siku hiyo atapanda ulingoni kutoana jasho na mkali wa Bongo Movie Jacob
Steven ‘JB’
Mbunge wa Kawe
(Chandema), Halima Mdee ameanza maandalizi yake ya pambano la ngumi
dhidi ya staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper.
Pambano la wakali
hao litafanyika Julai 7, siku ya Sabasaba katika Tamasha la Matumaini
kwenye Uwanja we Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo mwaka jana Wolper alionyesha uwezo kuliko Wema Sepetu katika pambano lao lililosisimua.
Lakini Mdee ametamba kumpoteza Wolper katika pambano lao hilo la Julai 7.
Mdee anaendelea na mazoezi mjini Dodoma, wakati Wolper anaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI HII NI SALEHJEMBE.BLOGSPOT.COM
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment