SUGU APATA DHAMANA NI BAADA YA KUTIWA ROKAPU KUTOKANA NA KUMWITA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA "MPUMBAVU" MJINI DODOMA.
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.
Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhoj
iwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.
Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
Hivi karibu Sugu aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kwamba "Tanzania haijawai kuwa na Waziri Mkuu 'Mpumbavu' anayetoa tamko la kuchochea Jeshi la Polisi kupiga raia".
Habarimpya.com imemtafuta msemaji wa Jeshila Polisi Tanzania ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kukamatwa kwa Mbunge huyo kupitia simu yake ya mkononi lakini hakupatikana.
0 comments:
Post a Comment