MECHI ya mchujo ya Kombe
la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu)
imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kam
a ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji
tiketi ni sh. 7,809,104. Asilimia
15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh.
83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 20,886,282.09.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment