Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu mlipuko uliotokea katika
mkutano wa Chadema uliofanyika katika Uwanja wa Soweto Kata ya Kaloteni
Mjini Arusha juzi. Picha na Venance Nestory.
DAR ES SALAAM/MIKOANI.
MLIPUKO wa bomu uliotokea Arusha na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 70 limezua utata kutokana na hisia tofauti za viongozi mbalimbali nchini waliozungumzia suala hilo, huku Rais Jakaya Kikwete akisema haamini kama Watanzania sasa wamefikia hatua ya kuanza kuhasimiana kwa misingi ya kisiasa.

Hii ni mara ya pili kwa Jiji la Arusha
kushambuliwa kwa bomu baada ya lile lililorushwa kwenye Kanisa la
Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi kwenye Parokia ya Olas
iti wakati wa sherehe ya uzinduzi wake Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu na kujeruhi 64.
Wakati Rais Kikwete akisema hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wamesema tukio hilo ni la kisiasa na lilipangwa.

Kufuatia tukio hilo, uchaguzi wa kata nne za Arusha mjini umeahirishwa hadi Juni 30.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana imeeleza kuwa
Rais Kikwete ambaye yuko nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa nchi
zilivyoendelea kiviwanda(G8), alisema haamini kama Watanzania ama
wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kudiriki kufanya
matukio ambayo yanahatarisha usalama wa watu.
“Mimi siamini kuwa Watanzania au wafuasi wa
vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kufanyiana matendo ya unyama wa
aina hii. Naamini kuwa hiki ni kitendo cha mtu ama watu wasioitakia mema
nchi yetu, watu ambao wanatafuta kila sababu ya kupandikiza chuki
miongoni mwa raia ama makundi ya raia, ili nchi yetu iingie kwenye
machafuko makubwa.”
Mbowe
Akizungumzia suala hilo, Mbowe alisema shambulio
hilo la bomu ni la kisiasa na lililenga kumuua yeye na Mbunge wa Jimbo
la Arusha, Godbless Lema.
“Haya ni mauaji ya kisiasa ya kupanga, tumeokota
maganda ya risasi za bastola na SMG na tumepiga picha na kuwapa polisi
katika eneo la tukio, gari letu lilipigwa mlango na vioo kwa risasi na
kesho wabunge wote wa Chadema watakuwa hapa Arusha na wataondoka baada
ya mazishi,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema pia wamebaini bomu lililorushwa ni
la kiwandani na shambulizi hilo liliandaliwa na kikosi cha watu wengi
wenye lengo la kufanya mauaji makubwa.
Alisema kilichomwokoa na kifo ni kushuka jukwaani
saa 11:43 kabla ya muda wa kawaida wa saa 12:00 kwani ilipangwa
washambuliwe wakiwa juu ya jukwaa.
“Tunasikitika sana, watu wamekufa wasio na hatia
na msiba huu utakuwa wa kitaifa na tunatarajia kuaga miili katika uwanja
huohuo wa Soweto,” alisema Mbowe.
0 comments:
Post a Comment