Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
DAR ES SALAAM:
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kama mfumo wa Serikali tatu utakubalika, Serikali ya Muungano haitakuwa na haja ya kukopa fedha.
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kama mfumo wa Serikali tatu utakubalika, Serikali ya Muungano haitakuwa na haja ya kukopa fedha.
Amesema hata katika suala la uwakilishi wa nchi
Kimataifa, Rais wa Muungano ndiye atakuwa na jukumu hilo na siyo Rais wa
Tanzania bara (Tanganyika) au Zan
zibar na kwamba Serikali hiyo ndiyo itakuwa na nguvu na itategemewa sana na Serikali nyingine.
zibar na kwamba Serikali hiyo ndiyo itakuwa na nguvu na itategemewa sana na Serikali nyingine.
Tangu Tume hiyo ilipotoa rasimu ya Katiba, watu wa
kada mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao, huku wakionyesha wasiwasi
mkubwa juu ya uendeshwaji wa Serikali hizo, kwamba utakuwa wa gharama
kubwa kuliko ilivyo sasa.
Katika mahojiano yake na waandishi waandamizi wa
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti
ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, Sunday Citizen na
Mwanaspoti, Tido Mhando ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL na Theophil
Makunga, Meneja wa Uendelezaji wa Biashara wa MCL, Jaji Warioba alitoa
ufafanuzi juu ya suala hilo.
Swali: Gharama za uendeshaji wa Serikali hizi
utakuwaje, huoni kama Rais wa Muungano atategemea zaidi fedha na msaada
kutoka Tanganyika na Zanzibar ?.
Warioba: Katika Katiba ya sasa mapato ya Muungano
yanatokana na vyanzo vitatu, Kodi ya Mapato (income tax), Ushuru wa
Forodha (custom duty) pamoja na ushuru wa bidhaa (excise duty).
Kodi ya mapato ndiyo inatoa fedha nyingi sana na
inafuatiwa na kodi ya ushuru wa bidhaa na ushuru wa forodha.
Kutokana na hesabu tulizopiga, tumeona matumizi katika Serikali ya Muungano yapo katika sehemu mbili, moja ni yale ya Muungano na ya pili ni yale ya Tanganyika ambayo yanachukua fedha nyingi.
Kutokana na hesabu tulizopiga, tumeona matumizi katika Serikali ya Muungano yapo katika sehemu mbili, moja ni yale ya Muungano na ya pili ni yale ya Tanganyika ambayo yanachukua fedha nyingi.
Mwaka 2010/2011 mapato ya kodi ya mapato yalikuwa
Sh2 trilioni na mapato ya ushuru wa bidhaa yalikuwa Sh1trilioni na
mapato ya ushuru wa forodha yalikuwa Sh600 bilioni.
Ni kwamba matumizi ya mambo ya Muungano yalikuwa
chini ya Sh1trilioni, ndiyo maana tumechagua ushuru wa bidhaa, kwani
tukipata fedha zile zitaweza kumaliza matumizi yote ya Serikali ya
Muungano.
Hivyo basi kama tukiendelea na utaratibu huu wa
Serikali tatu, ni wazi kwamba Serikali ya Muungano haitakuwa na haja ya
kukopa fedha kwa kuwa itakuwa nazo za kutosha, Serikali zitakazokopa ni
hizo mbili.
Tulikuwa tukijua wazi kuwa Serikali ya Muungano
lazima iwe na chanzo cha uhakika cha fedha, na kwa utaratibu huu
Serikali hizo tatu ndizo zitakazokubaliana jinsi ya kukusanya fedha
hizo.
Swali: Rais yupi atakuwa na madaraka katika mfumo wa Serikali tatu ?. CHANZO MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment