Katika
kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi
linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua
stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria
vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali
zikiwemo maeneo ya biashara.
Ikumbukwe
kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia
muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye
maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu
hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya
uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu.
Jeshi la Polisi
limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu
hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya
uvunjifu wa amani.
Ulinzi
umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za
starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa
ya watu.
Aidha,
wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa
kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari
na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi
wanatakiwa kuwa makini hususani watokapo kwenye makazi yao, wasiache
nyumba wazi ama bila mtu na pale inapobidi watoe taarifa kwa majirani
zao. Wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe
taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
Vilevile,
Jeshi la Polisi linawatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli
yanayotumia majina ya viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa
ili kujipatia pesa na vitu mbalimbali. Matapeli hao wamekuwa wakitumia
ujumbe mfupi wa simu za mkononi kupata taarifa za mtu binafsi hatimae
mtu huyo kuibiwa.
Ndugu wanahabari,
Kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo, pamoja na watu wote wanaoingia ama kuishi na kufanya shughuli hapa nchini bila kufuata utaratibu (wahamiaji haramu) kutakiwa kuondoka au kuharalisha ukaazi wao, Jeshi la Polisi linawataka watu hao kuendelea kutekeleza agizo hilo la Serikali kabla ya Operesheni kabambe kuanza itakayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama.

baadhi ya watu hao tayari wamekwishasalimisha silaha wanazozimiliki
kinyume cha sheria na pia baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kuondoka
hususani katika mikoa ya Kagera na Kigoma. Hiyo ni hatua nzuri,
tunawataka wale wote ambao bado hawajatekeleza agizo hilo, waendelee
kufanya hivyo haraka kabla ya muda wa msamaha kumalizika.
Mwisho,
napenda kuwahakikishia wananchi kwamba, Jeshi la Polisi linatekeleza
majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika
kumwonea huruma ama upendeleo mtu yeyote atakayeenda kinyume na sheria.
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA
EID –EL-FITR
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA
EID –EL-FITR
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment