BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA KIJESHI YALIPUKA NA KUTEKETEA KWA MOTO WAKATI IKITUA KWA DHARURA NA KUUA SOMALIA

Ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.MOJA YA NDEGE ZA NCHI YA SOMALIA.Ndege ya kivita MaliPICHA YA NDEGE ZA JESHI YA MAKTABA SIO YA SOMALIA.

NDEGE ya kijeshi imelipuka na kuteketea nchini Somalia baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Mogadishu.

Kikosi cha muungano wa Afrika nchini Somalia ambacho kina kambi yake katika uwanja huo wa ndege kimesema kuwa wanajeshi wake kadhaa wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa.

Inasemekana kuwa ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.
Kuna ripoti kuwa ndege ilikuwa imebeba zana za kivita.
Wafanyakazi katika uwanja huo wa ndege waliel
ezea kusikia milipuko kadhaa huku moto ukienea kwa ndege hiyo.

Ndege za kijeshi hutua katika uwanja huo wa ndege unaotumiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika wanaopambana dhidi ya wapiganaji wa Al shabaab wanaosemekana kuwa na uhusiano na al Qaeda.

Wakati huohuo, kwenye mtandao wao wa Twitter kundi la Al Shabaab limeeleza kufurahia kwa kulipuka kwa ndege hiyo hasa kwa kuwa ililipuka yenyewe. 

Kwenye ujumbe mwingine , kundi hilo lilisema kuwa ndege hiyo iliyokuwa imebeba silaha iliteketea katika uwanja wa Mogadishu na kuharibu kila kilichokuwa kwenye ndege yenyewe. 

Kundi hilo lililaumu ilichokiita watu waliolaaniwa kwa kupanga mauaji ya waumini na kufanya uharibifu lakini kila wanachokifanya, juhudi zao zinagonga mwamba. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: