Mhe Sitta.
Mhe Mary Pius Chatanda.Dar es Salaam.
WIKI moja baada ya kukaririwa akisema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo na kwamba hawana mchango wowote bungeni na wala hawatembelei majimbo yao wakisubiri kubebwa na chama, Spika wa Bunge wa zamani, Samuel Sitta amewageukia wabunge wa Viti Maalumu akisema hawana umuhimu wowote.
Akizungumza kwa simu juzi, Sitta ambaye sasa ni
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema: “Ninakerwa sana na
mfumo wa Viti Maalumu, kwanza sioni umuh
imu wa mfumo huu kuendelea kuwepo katika Katiba Mpya. Hawana umuhimu wowote.”
imu wa mfumo huu kuendelea kuwepo katika Katiba Mpya. Hawana umuhimu wowote.”
Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Uwanja
wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu Julai 29,
mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama, Sitta
aliwajia juu bila ya kuwataja baadhi ya wabunge wa CCM.
“Wanakwenda bungeni hawachangii, hawana hata hoja
za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta na
kuongeza: “Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda
kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... Inawezekana
hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa
wakiomba tena kura.”
“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta
mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa
wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana
hawayajui lakini watu hawaendi jimboni, wananchi watayafahamu vipi haya
maendeleo?”
Juzi, akizungumzia wabunge wa Viti Maalumu, Sitta
alisema... “Wengi wao hawachangii chochote na mbaya zaidi hakuna wa
kuwahoji chochote kama wabunge wanavyorudi jimboni.
“Ikifika wakati wa posho wapo. Sisemi kama naumia
wao kuchukua posho.... hawa wanachukua posho wanawajibika kwa nani? Nani
anahoji utendaji wao na zaidi itakapokuja Katiba Mpya ya kuwawajibisha
wabunge wazembe, hawa watawajibishwa wapi?”
“Rasimu ya Katiba Mpya isiwaruhusu hawa... hawa
nao ni mzigo mwingine. Wakifika bungeni hawachangii chochote, hawawezi
kuwajibishwa na yeyote kwa mfumo uliopo na pia hawawajibiki popote, sasa
huu si mzigo?”
Walikwishaanza mkakati
Hata hivyo, Juni 9, mwaka huu, ikiwa ni wiki moja
baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
kutangaza Rasimu ya Katiba huku ikifuta Viti Maalumu, wabunge wanawake
walianza kuweka mikakati ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa lengo la kukamata
majimbo.
Kwa mara ya kwanza, wabunge hao wa Viti Maalumu
walikutana kwa siku mbili kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa, Dodoma lengo
likiwa ni kujadili mikakati mbalimbali ya kupambana jimboni.
Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake, Anna Abdallah
alisema wanaweka mikakati kuwawezesha kusimama wenyewe kwenye majimbo
mwaka 2015 hasa baada ya kufutwa kwa Viti Maalumu katika rasimu. MWANANCHI.
Mhe. Gaudentia Mugosi Kabaka ( MB) Waziri wa Kazi na Ajira akizungumza wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
WABUNGE wa viti maalumu CCM ni pamoja na viongozi wakuu wawili wa jumuiya ya wanawake wa chama hicho (UWT), ambao ni mwenyekiti wake, Sophia Mnyambi Simba na katibu wake, Amina Nassoro Makilagi.
Wengine ni Gaudentia Mugosi Kabaka, Ummi Ally Mwalimu, Agnes Elias Hokororo, Martha Jachi Umbulla, Lucy Thomas Mayenga na Faida Mohamed Bakari.
Walioteuliwa wengine ni Felista Alois Bura, Kidawa Hamid Saleh, Stellah Martine Manyanya, Maria Ibeshi Hewa, Hilda Cynthia Ngoye, Josephine Johnson Genzabuke na Esther Lukago Midimu.
Wengine ni Maida Hamad Abdallah, Asha Mshimba Jecha, Zarina Shamte Madabida, Namalok Edward Sokoine, Munde Tambwe Abdallah, Benardetha Kasabago Mushashu, Vick P. Kamata, Pindi Hazara Chana, Fatuma Abdallah Mikidadi, Gertrude Rwakatare, Betty E. Machangu, Diana Mkumbo Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Matitu Vulu, Abia Muhama Nyabakari, Pudenciana Kikwembe, na Lediana Mafuru Mng’ong’o.
Walioteuliwa wengine ni Sarah Msafiri Ally, Catherine V. Magige, Ester Amos Bulaya, Neema Mgaya Hamid, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Dkt. Fenella E. Mukangara, Terezya Lwoga Huvisa, Al-Shaymaa Kwegir na Margreth Mkanga.
Angellah Jasmin Kairuki, Zainab Rashid Kawawa, Mwanakhamis Kassim Said, Riziki Said Lulida, Devotha Mkuwa Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Salum Mfaki, Margreth Simwanza Sitta, Subira Khamis Mgalu, Rita E. Kabati, Martha Moses Mlata, Maua Abeid Daftari na Elizabeth Nkunda Batenga.
Wamo pia, Azza Hillal Hamad, Mary Machuche Mwanjelwa, Josephine T. Chengula, Bahati Ali Abeid, Kiumbwa Makame Mbaraka, Roweete Faustine Kasikila, Anastazia Wambura na Mary Pius Chatanda.

0 comments:
Post a Comment