MAMIA ya wahamiaji haramu kutoka nchini Rwanda wakiwa na ng’ombe zaidi 900 wameanza kuondoka nchini kurejea kwao kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwataka waondoke Tanzania kabla ya siku 14.
Aidha, imeelezwa kuwa kumekuwapo ongezeko la
askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mkoani Kagera hasa
wilayani Ngara hali inayozua hofu kwa baadhi ya wananchi, huku ikiongeza
msukumo kwa wahamiaji haramu kuond
oka.
oka.
Akiwa katika ziara mkoani Kagera, Rais Kikwete
alitoa agizo la kuwataka wote waliokuwa wakiishi nchini kinyume cha
sheria waondoke mapema jambo lililotakiwa kuanza kutekelezwa Julai 29 na
kukamilika Agosti 10 mwaka huu.
Alisema kuwa wahamiaji haramu na wale wanaoendesha
ama kuhusika na ujambazi, uhamiaji haramu na uingizaji haramu wa mifugo
waamue kuchukua hatua mwafaka za kuondoka mapema kabla vyombo vya
ulinzi na usalama kuanza operesheni maalumu ya kuwasaka.
Tayari idadi kubwa ya wafugaji wenye makundi ya
ng’ombe imeanza kuondoka kuelekea eneo la mpakani la Rusumo kutoka ardhi
ya Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa agizo hilo la Rais Kikwete.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya
simu, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costantine Kanyasu alisema kwamba idadi
kubwa ya wafugaji waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria, imeitikia wito
wa agizo la Rais na kuanza kuondoka kwa hiyari yao.
Hata hivyo, alisema kuwa pamoja na idadi kubwa ya
wahamiaji kuanza kuondoka, bado wapo ambao hawajaondoka kutokana na
kudai kuwa na vibali walivyovipata kutoka Ofisi ya Uhamiaji na
kubainisha kwamba vibali hivyo vitakaguliwa kwa umakini wakati wa
operesheni maalumu ili kujua uhalali wake.
“Jambo hili la wahamiaji haramu lilikuwa kero
kubwa, siyo tu kwa Wilaya ya Ngara, bali mkoa mzima wa Kagera, lakini
tunashukuru sasa wameanza kuondoka, wamebaki hao wenye vibali. Ni lazima
vibali hivyo tutavikagua maana vipo vilivyotolewa kinamna,” alieleza
Kanyasu.
Alionya kwamba jukumu la kuwaondoa kwa nguvu
wahamiaji haramu pamoja na wafugaji linasubiri muda wa mwisho ili kuanza
kutekelzwa kama Rais Kikwete alivyoagiza.
Hofu ya Wanajeshi kuongezeka
Akizungumzia suala la wanajeshi kudaiwa kuongezeka
wilayani Ngara, Kanyasu alisema kwamba katika wilaya yake kuna kikosi
cha dharura kinachokaa katika moja ya kambi za JWTZ kikikuwa na idadi
kubwa ya askari lakini wananchi hawakuwa na taarifa nacho ila kutokana
na sababu za kiusalama.
“Unajua kuna kelele za hapa na pale na haya
majibizano yanayotokea baina ya Rwanda na Tanzania. Haya ni kama
yamewastua watu na kudhani kuwa askari wetu wa Kikosi cha Dharura
waliopo hapa Ngara wameletwa maalumu kutokana na tahadhari,” alisema na
kufafanua kuwa askari hao wapo siku zote kwa ajili ya kulinda mipaka ya
Tanzania.
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kutulia na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo. MWANANCHI
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kutulia na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment