BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ACHA KABISA MAMBO YA KUPENDA, RAIS OBAMA NA MKEWE MICHELLE OBAMA WAVURUGUNA MKASA PITIA HII HABARI.



NDOA ya Michelle na Barack Obama yaweza kuvunjika kwa talaka kutokana na mapito magumu ambayo ndoa hiyo ilipitia na bado inaendelea kupitia.


Michelle Obama amechoshwa na ndoa yake na Obama. Kutokana na ripoti iliyotolewa na Bombshel , Mitchel na Obama wamekuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya Ikulu (White house). Michelle pia anajiandaa kuhama katika jumba lao pale Chicago ambalo wameishi wakati wa uchumba wao miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo watajadili juu ya talaka.


Tatizo limeanza miaka nane iliyopita pale Obama alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao Sasha ambaye anumwa ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal Meningitis ndio uliowafanya waendelee kuwa pamoja.


Kitabu cha Anderson kinaelezea ndoa ya Mitchel na Obama kama ndoa halisi ya Wamarekani ikielezea tatizo lilivyoanza baada ya Barack Obama kuamua kuingia kwenye siasa. Alisikika Mitchel, 48 mara kadhaa akimwambia mume wake “Wewe unajifikiria mwenyewe tu”



Naye Barack Obama amesikika akisema:
“Sikuwahi kufikiri kamwe kwamba ningelea familia mwenyewe siku moja”

Anderson anadai kuwa Obama amechoshwa na malalamishi ya mke wake



“Nampenda sana Michelle lakini ananiumiza na ubishi wake wa kila mara” Barack Obama alisikika akiongea hivyo na bibi yake Madelyn Dunham



“Anaonekana tu mwingi wa machungu, na hasira siku zote”

 

Anderson pia anafunua siri ya ugonjwa wa moyo ambayo Mitchel alikuwa nayo kabla hajajifungua mtoto wao wa kwanza. Akizungumza na CBS Anderson anadai kuwa ilikuwa nusura Mitchel atembee nje ya ndoa kwa sababu ya upweke.




Kipindi cha useneta wa Barack Obama kilikuwa ni kipindi kigumu na cha giza nene kwenye ndoa yao.




Kwa miaka mitano wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wao wa kupata watoto kabla Malia hajazaliwa. Walishajadili sana suala la kuridhi watoto (adoption) na marafiki zake wa karibu lakini kwa bahati nzuri Malia akazaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.




Wanandoa hawa wamekuwa wakipitia katika mapito magumu ya ndoa yao na wamekuwa pamoja tu kwa sababu ya mtoto wao na itifaki ya kisiasa.




Mwandishi huyo anadai Barack Obama na Mke wake Michelle ambao wanaenda kusheherekea miaka 17 ya ndoa yao mwezi ujao wa January 2014 kuwa ndoa yao iko imara kwa sasa.




Lakini vyanzo vingine vya taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara, hasa baada ya tukio la Obama kupiga picha za pamoja bila aibu na waziri mkuu wa denmark, 46 kwa jina Helle Thorning-Schmidt wakati wa huduma yakumuaga aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrka ya Kusini, Bwa Neslon Madiba Mandela. Obama, 52 alikuwa akicheka na kumnong’oneza waziri huyo kwa muda wote kwenye sherehe hiyo maalumu kwa viongozi wa dunia huku Michelle akiwa pembeni yake amenuna tu.















Mara nyingi alikuwa akimshika shika mabega yake na kumuudhi zaidi na zaidi Michelle.




“Lakini sasa Michelle ni kichaa kama jehanamu, anajiona kanyanyasika mbele ya dunia kwani picha hizo zilirushwa duniani kote kwenye Television, magazdeti na mitandao mbalimbali. Alisikika akimtapikia mume wake huku akisema “Nimechoshwa” “Alikutana na mwanasheria wake wa talaka na kamwambia Barack Obama kuwa anataka maisha nje nay eye. Michele amekusudia kubaki whitehouse mpaka Obama amalize muda wake uliobakia kwa ajili ya maonyesho tu lakini ameweka wazi kuwa kila mtu ataishi maisha yake baada ya hapo.




Msemaji wa ndani ya ikulu anaendelea kusema kuwa Barack Obama amechoshwa sana na mpango wa afya wa hivi karibuni ulioleta mvutano ndani ya bunge la Marekani na sasa anakutana na tatizo jingine kubwa zaidi la Michelle juu ya ndoa yake.




“ Michelle kwa upande wake anahamia kwenye mojawapo ya vyumba tupu kwenye nyumba yao ya kifamilia ya binafsi na anajiandaa kuamisha nguo zake nje ya jumba lao la mamilioni ya dola pale Chicago




Pia tatizo limekuzwa na safari ya kikazi ya Obama hivi karibuni kule Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri Mkuu mrembo kuliko pengine wote duniani , Yingluck Shinawatra picha zake ziko hapo chini ambaye anasadikiwa kuwa anampenda Obama.











Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: