BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAWA NDIYO WANAOMFUKUZA MHE ZITTO ZUBERI KABWE NDANI YA CHADEMA.

ZITTO KABWE.

Dar es Salaam,Tanzania.
WAKATI sinta fahamu kuhusu sakata la Kamati Kuu ya Cha Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumfukuza katika safu ya Uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe,taarifa za ndani ya Chama hicho zinaeleza kwamba Mbunge huyo wa Kigoma amefukuzwa uachama.



Taarifa zinaeleza kwamba ingawa kuna mvutano mkubwa kuhusu kufikia uamuzi huo,ila wajumbe wa Kamati Kuu wamezidia nguvu na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Willbrod Slaa ambao wamegoma katakata kuwasamehe watuhumiwa hao huku wakisema kwamba kitendo cha kuwa samehe itaongeza uhaini ndani ya Chama. 



Inaelezwa kwamba hatua hiyo pia ili sababisha mwasisi wa Chama hicho Mzee Edwin Mtei kuingilia kati suala hilo, lakini akazidiwa nguvu na wawili hao kwa hoja kwamba Zitto akisamehewa Chadema itakufa,hivyo ni bora akafukuzwa ili wabaki na kazi moja ya kukijenga Chama mapema kabla ya kufika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.



Wakati hayo yakiendelea taarifa zaidi zilizonaswa na Habarimpya.com zinaeleza kwamba hatua ya Mbowe kushikilia msimamo wake wa kumtimua Zitto uanachama inatokana na tuhuma zilizo ibuliwa na Mbunge huyo hivi karibu kwamba yeye ni mmoja wa mafisazi walioficha fedha nje ya nchi akishirikiana na mafisadi wengine, ambao wametumia vyema fedha zao ndani ya Chadema ili kuhakikisha kwamba Zitto anang'olewa.



Baadhi ya mafisadi mbalimbali wanaotajwa katika tuhuma za kuhakikisha Zitto anafukuzwa uanchama, kabla ajakamilisha hazma yake ya kuwataja watuhumiwa walioficha mabilioni nje ya nchi ni pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media Regnard Mengi,Rostan Azizi pamoja na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja. 



Wakati hayo yakiendelea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, hivi karibuni walihojiwa kuhusu kuwa na utajiri mkubwa nje ya nchi. 



Wanasiasa hao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na serikali hivi karibuni, kwa ajili ya kutafuta mali mbalimbali zilizofichwa nje ya nchi na watu mbalimbai wenye nyadhifa kubwa. Kwa habari zaidi ya ufisadi wa Mbowe na wenzake bofya maandishi ya bluu hapo mbele,

ZITTO AMPONZA MBOWE, AKUMBWA NA KASHFA ZITTO.
Jackson Odoyo,Dar es Salaam

SAKATA la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo. 




Wakati hayo yakiendelea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz, wamehojiwa kuhusu kuwa na utajiri mkubwa nje ya nchi. Wanasiasa hao wamehojiwa na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na serikali hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta mali mbalimbali zilizofichwa nje ya nchi na watu mbalimbai wenye nyadhifa kubwa. 



Kikosi kazi hicho kiliundwa baada ya Zitto Kabwe kutangaza kwamba kuna watanzania wameficha fedha katika nchi mbalimbali duniani huku akiitaja Uswisi kuwa ni miongoni mwa nchi hizo. Taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com zinaelezwa kwamba mbali na wanasiasa hao kuhojiwa na kikosi hicho pia kuna idadi kubwa la vijana wasiojihusisha na siasa waliohojiwa. 



Kuhojiwa kwa vijana hao inaelezwa kwamba ni kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo imebainika kwamba inawapa vijana wengi utajiri wa muda mfupi huku kundi kubwa la watumiaji wa dawa hizo wakizidi kuharibikiwa huku jina la Tanzania ikiendelea kuchafuka kimataifa. 



Mbali na taarifa hizo Gazeti la Raia Mwema la Tanzania pia ili ripoti kuwa Kikosi hicho kiliundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kinaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah na wawakilishi kutoka Jeshi la Polisi, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na waatalamu wa masuala ya kibenki.


Chanzo cha kuaminika kilisema Mbowe ambaye pia ndiye Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alihojiwa kutokana na maelezo kuwa alinunua jumba la kifahari nchini Dubai, Desemba mwaka 2011. 



“Kutokana na wadhifa wake kwa umma, Mbowe ilibidi achunguzwe kutokana na ununuzi wa nyumba alioufanya nchini Dubai, Desemba mwaka 2011. Uchunguzi wake ni mahususi kwa sababu tumefuatilia akaunti zake na ikaonekana hakuwahi kutumia njia ya benki kufanya malipo. 


“Hii maana yake ni kwamba kama alifanya malipo, basi alifanya kwa kutumia fedha taslim (cash). Sasa ni lazima ichunguzwe maana si kawaida kwa kiongozi kama yeye kusafiri na mamilioni yote ya kununua jumba kule Dubai na kulipa cash. Ndiyo maana yeye anafanyiwa uchunguzi mahususi,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hilo. 



Rostam ni miongoni mwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini na Raia Mwema limeelezwa kwamba alihojiwa kutokana na kumiliki jumba katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati na imeelezwa pia kuwa ana akaunti kadhaa nje ya nchi. 



Dubai ni kimbilio la wafanyabiashara wengi kutokana na nafuu ya kodi inayotolewa na serikali ya nchi hiyo na pia uwepo wa biashara na usalama mkubwa uliopo. Zaidi ya kuwa mfanyabiashara maarufu, Rostam aliwahi kuwa mbunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alipata pia kuwa Mweka Hazina wa chama hicho. http://www.habarimpya.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: