Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela lilipofikishwa Uwanja wa Ndege wa Mthatha jana.
Maziko yanafanyika leo kijijini kwao, Qunu kwa taratibu za kimila. PICHA
| AFP.
QUNU.
HUZUNI na simanzi viliyateka maeneo ya Mthatha na Qunu katika Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini baada ya kuwasili kwa mwili wa rais wa kwanza mzalendo wa nchi, Nelson Mandela.
QUNU.
HUZUNI na simanzi viliyateka maeneo ya Mthatha na Qunu katika Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini baada ya kuwasili kwa mwili wa rais wa kwanza mzalendo wa nchi, Nelson Mandela.
Mwili wa Mandela uliwasili jana katika Uwanja wa
Ndege wa Mthatha saa 7:40 mchana (kwa saa za huku) dakika 20 kabla ya
muda uliotarajiwa, ukiwa umesafirishwa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jeshi
wa Waterkloof, Pretoria.
Ulisindikizwa na maofisa waandamizi wa Jeshi la
Afrika Kusini (SANDF), maofisa kutoka Serikali, wawakilishi wa familia
yake na viongozi wa mila kutoka kabila la abaThembu.
Mandela anazikwa leo katika makaburi ya familia
yaliyopo katika Kijiji cha Qunu ambako alikulia, katika mazishi ambayo
yatakuwa mchanganyiko wa mila na desturi, dini yake ya Kikristo ikifuata
taratibu za kimethodisti na kijeshi kwa maana ya Serikali.
Alizaliwa katika Kijiji cha Mvezo, Julai 18, 1918
na alifariki dunia Desemba 5, mwaka huu nyumbani kwake, Houghton,
Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuugua magonjwa ya figo
kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Maziko yake yanamaanisha kuhitimishwa kwa siku 10
za maombolezo ya kitaifa, ambayo yalishuhudia mamia ya viongozi kutoka
pande zote za dunia, waliofika Afrika Kusini kushiriki Ibada ya Kitaifa
iliyofanyika katika Uwanja wa FNB, Soweto Jumanne iliyopita.
Kadhalika mwili wa kiongozi huyo kwa siku tatu
mfululizo; Jumatano hadi Ijumaa wiki hii ulikuwa ukiwekwa katika Ikulu
ya Pretoria iliyopo Majengo ya Umoja (Union Buildings) ambako
waombolezaji zaidi ya 100,000 walipata nafasi ya kutoa heshima zao za
mwisho.
Serikali ya Afrika Kusini imetaganza kuwa leo ni
siku ya mapumziko huku wamiliki wa maduka makubwa nao wakitangaza kwamba
hawatafungua biashara zao kama hatua ya kuienzi siku ya mwisho ya
Mandela.
Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Malawi, Joyce
Banda ni wakuu wa nchi pekee ambao watahudhuria mazishi ya Mandela na
wote wamepangiwa kutoa salaamu za rambirambi wakati wa mazishi.
Watawaongoza viongozi wengine kadhaa wakiwamo wale wanaowakilisha
mashirika ya kimataifa.
Simanzi uwanjani
Uwanja wa Ndege wa Mthatha ulikuwa kimya hasa
baada ya ndugu wa karibu wa Mandela, wakiongoza na mjane Graca Machel
kuwasili saa 6:44 mchana na kulakiwa na viogozi mbalimbali wakiongozwa
na Waziri wa Ulinzi, Nosiviwe Mapisa Nqakula.
Mara baada ya jeneza kushushwa kutoka kwenye ndege
ya jeshi Namba C-130, wimbo wa taifa ulipigwa, pia kupokea heshima
kutoka kwa askari wa SANDF ambao walikuwa uwanjani hapo mapema. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment