BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WABAKA WANAWAKE KABILA LA ROHINGYA.

HABARI ZA KIMATAIFA.Rohingya Muslim women cry after attack of village
WANAWAKE Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar, wanakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na maafisa usalama katika vituo vya polisi nchini humo.
 

Kwa mujibu wa ripoti maafisa wa usalama nchini Myanmar wamekuwa wakiwateka nyara wanawake na wasichana Waislamu wa kabila hilo sanjari na kuwapiga na kuwatukana. 


Habari zinasema kuwa, baada ya maafisa hao kuwalazimisha kutumia madawa ya kulevya huwapeleka katika vituo vya usalama na kuwabaka bila ya wao kujielewa. 


Hii ni katika hali ambayo jamii ndogo ya Waislamu nchini humo imekuwa ikinyimwa haki zake za kimsingi kutokana na serikali ya Naypyidaw kupinga kuwapa Waislamu wa jamii hiyo haki yoyote kwa madai kuwa eti sio raia wa nchi hiyo. 


Aidha kwa mara kadhaa Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki za binaadamu yamekuwa yakiituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia vimavyofanywa na maafisa wa usalama na jeshi dhidi ya wanawake Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo. CHANZOhttp://kiswahili.irib.ir
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: