BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIBWEKA VYA KUFUNGA MWAKA 2013 !!! MAHAKAMA YAMHUKUMU KIJANA KIFUNGO CHA SIKU 45 KWA KUTENDA KOSA LA KUSALI KATIKA MSIKITI ULIOBOMOLEWA.

Mtoto Yaaqub Nahdi Aref (2) akiwa katika sala ya Idd el Fitri na waumini wa dini ya kiislam inayosaliwa kufuatia kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo waumini wa dini ya kiislam wanaungana na waislam wenzao duniani kote kusherehea sherehe za sikukuu hiyo hapa nchini iliyofanyika kwenye viwanja vya The Islamic Foundation kata ya Boma mkabara na hoteli ya Hilux Manispaa ya Morogoro. PICHA YA MAKTABA/MTANDA BLOG


MAHAKAMA ya Bahrain imemhukumu kijana mmoja wa nchi hiyo kifungo cha siku 45 jela kwa kosa la kusimamisha Sala katika msikiti uliobomolewa na utawala wa kifalme wa Aal Khalifa nchini humo.



Taarifa kutoka Manama zinaeleza kuwa, Ali Hashim Ali alipatikana na hatia hiyo ya kusali katika Msikiti wa Muhammad Amir al Barighi ulioko nje kidogo ya Manama mji mkuu wa nchi hiyo. 


Kikosi cha Usalama nchini Bahrain kwa muda wa wiki mbili kimekuwa kikilizingira eneo la msikiti huo uliobomolewa na kuwapiga marufuku Waislamu kutekeleza ibada zao katika eneo hilo. 


Hatua ya utawala wa kifalme wa Aal Khalifa kuwakataza Waislamu wasitekeleze ibada ya sala katika eneo hilo imewakasirisha wananchi wa nchi hiyo ambayo zaidi ya asilimia 99. 8 ya wakazi wake ni Waislamu.


Inafaa kukumbusha hapa kuwa, tokea ilipoanza harakati ya wananchi wa Bahrain mwezi Februari 2011 hadi sasa, mamia ya wapinzani wa serikali wameuawa na kutiwa mbaroni na zaidi ya misikiti 50 imebomolewa na askari usalama ya nchi hiyo. 


Vilevile utawala huo wa kifalme umetakaa katakata kukarabati au kujenga upya misikiti hiyo iliyobomolewa.http://kiswahili.irib.ir
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: