BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIRI YA YANGA KUSITISHA MKATABA KWA KOCHA MKUU WA KLABU HIYO MHOLANZI ERNRST BRANDTS NDIYO HII.


YANGA imetangaza rasmi kusitisha mkataba na kocha Mholanzi, Ernest Brandts, kwa kumpa notisi ya siku 30 na Mwanaspoti linafahamu kwamba Boniface Mkwasa ndiye anatarajiwa kuwa Kocha Msaidizi mpya akichukua nafasi ya Fred Minziro.




Sababu kubwa zilizotajwa na uongozi ni kushindwa kwa Brandts kufanya kazi kwa ufanisi. Hata hivyo habari za ndani zinadai mzozo wake na mastraika, Hamis Kiiza (pichani) na Didier Kavumbagu, ndio kisa cha yeye kung’olewa.


Kocha huyo alitofautiana na wachezaji hao kwenye mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Mgambo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaaam ambapo Kiiza alitolewa dakika ya 45 na akakasirika na kumshutumu hadharani kocha huyo wakati timu ikielekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Mchezaji huyo alidai kuwa Brandts amekuwa akiwapendelea baadhi ya wachezaji. Kwa Kavumbagu, naye alizozana na kocha huyo baada ya kutopangwa kwenye mechi hiyo.


Ingawa Kavumbagu aliomba radhi baadaye kwa maneno, lakini Kiiza hakuwahi kurekebisha kauli yake na habari za ndani zinadai kwamba alikuwa akiungwa mkono na baadhi ya wachezaji wenye ushawishi mkubwa kwa uongozi na mashabiki.


Kiiza mwenye mabao manane katika ligi, alitaka kucheza dakika zote 90 kwa lengo la kuongeza idadi ya mabao yake.


Habari za ndani zinadai baadhi ya viongozi waligawanyika kutokana na mzozo huo ambao ulimfanya Brandts akaanza kushindwa kuimudu timu.


Lakini uongozi huo ulitamka sababu ya kusitisha mkataba huo ni kutoridhishwa na kiwango cha uchezaji wa timu yao kwenye baadhi ya mechi na hasa ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba iliyochezwa Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa na Yanga kulala 3-1.


Brandts ambaye alichukua mikoba kutoka kwa Mbelgiji, Tom Santifiet, msimu uliopita alisaini mkataba mpya mwanzoni mwa mwezi huu ambao ungemfikisha Desemba mwakani.


Mwenyekiti Kamati ya Mashindano na Usajili, Abdallah Bin Kleb, alisema: “Jana (juzi Jumapili) tulikubalina kusitisha mkataba wa kocha wetu Brandts na tumempa notisi ya mwezi mmoja.


“Brandts atatumikia notisi kulingana na makubaliano ya mkataba kwa maana ataendelea kuifundisha timu kwa kipindi chote hicho ambapo nasi tutakuwa kwenye mchakato wa kumtafuta atakayerithi mikoba yake.


“Tunashukuru alipoishia, kwani alipofika Yanga kwa mara ya kwanza aliisaidia hadi tukachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara na aliinua kiwango cha timu.

KWA HABARI MOTO MOTO ZA MICHEZO NDANI NA NJE YA NCHI USIKOSE KUPATA NAKALA YA MWANASPOTI AU KUTEMBEA  http://www.mwanaspoti.co.tz
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: