Ni mbio za aina yake ambazo zilitia nakshi mashindano ya mbio za Baiskeli na Safari Lager mkoani Shinyanga. PICHA YA MAKTABA. |
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema juzi kuwa juzi, saa 7 mchana eneo la Kigogo-Mkwajuni, Mkani anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40, akiwa anaendesha baiskeli alionekana kuishiwa nguvu na alidondoka chini, hatimaye kufariki dunia papo hapo.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, sababu za kifo hicho bado hazijafahamika. Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.
Katika tukio jingine, Said Mtagaja aliyekuwa akiendesha gari T 242 CGD Faw, amefariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea juzi, saa 7 mchana wakati gari hilo likitokea Ubungo kuelekea Mbezi.
Kamanda Wambura alisema gari hilo lilipofika eneo la Kimara Mwisho kwenye kona kali lilimshinda dereva na kupinduka.
Alisema utingo wa gari hilo, Bakari Hassan, alijeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na amelazwa katika Hospitali ya Tumbi, maiti imehifadhiwa hospitalini hapo. TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment