BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IKULU YAFUNGA MJADALA KUHUSU MAWAZIRI MIZIGO, RAIS HAJAONA MIZIGO NDIYO MAANA AMEWATEUA, WAACHE WAFANYE KAZI.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.


DAR ES SALAAM.

IKULU imetaka kufungwa kwa mjadala wa kuhusu kurudishwa kwa mawaziri wanaodaiwa kuwa ni mizigo kwenye Baraza la Mawaziri na badala imetaka waachwe wafanye kazi.


Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema kuendeleza mjadala huo ni kupoteza muda, kwani Rais Jakaya Kikwete alishamaliza kazi yake.


Rweyemamu alisema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua mawaziri ambao wana wajibu wa kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake, hivyo si sahihi wateule hao kuitwa ‘mizigo’ kwani yeye (Rais) ameona wanafaa.


“Rais anapoteua watu anaangalia wanaofaa kumsaidia na si vinginevyo. Kwani lengo lake ni kuona nchi ina `move forward’ (inasonga mbele) kimaendeleo,” alisema Rweyemamu. Alisema watu wanapaswa kukumbuka kuwa mtu anapoteuliwa kwenye uwaziri kuna suala la uwajibikaji: “Anatakiwa kutekeleza uwajibikaji wa pamoja. Sasa kumshambulia mtu binafsi na kumwita mzigo siyo sahihi.”


Rweyemamu alisema mjadala huo kwa sasa umepitwa na wakati na kuwataka wananchi na wachambuzi kuwaacha mawaziri hao kuchapa kazi.


“Ni vizuri wananchi wakawapa nafasi mawaziri hawa ya kufanya kazi na baadaye kuwapima na kuwachambua kutokana na utendaji wao,” alisema.


Chimbuko la majadala


Mjadala kuhusu suala hilo unatokana na Rais Kikwete kuwarejesha katika Baraza la Mawaziri baadhi ya mawaziri ambao walidaiwa kuwa ni mizigo kutokana na udhaifu katika utendaji wao.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana na Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ndiyo walioasisi mawaziri hao kuwa ni ‘mizigo’ walipokuwa na ziara ya kikazi mkoani Ruvuma, mwishoni mwa mwaka jana.


Mawaziri waliolalamikiwa kutokana na utendaji wao ni wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo, Waziri wa zamani wa Fedha, marehemu Dk William Mgimwa na aliyekuwa Naibu wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.


Baadaye baadhi ya wabunge nao walikoleza moto kwa kushinikiza mawaziri hao wang’oke, huku wakiongeza idadi yao kwa kuwataja Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia na Manaibu wake, Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa katika kundi hilo.


Mawaziri hao waliitwa kujieleza mbele ya Kamati Kuu ya CCM kuhusu sababu za utendaji wao kuwa wenye matatizo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: