BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA VIWANDA NA UBINAFSISHAJI APATA AJALI KIBAHA PICHA YA NDEGE


Gari la Ngasongwa likiwa limeharibika vibaya jana. Picha na Chris Mfinanga


ALIYEKUWA waziri wa viwanda na ubinafsishaji, Mh Juma Ngasongwa akikokotwa kuingizwa Hospitali ya Tumbi kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali katika eneo la Kibaha jana jioni. Mhe. Ngasoma amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Dr Loti Kiwelu akimjulia hali katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipofikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili ya matibabu zaidi.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Rav 4 mali ya Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco pichani chini.

Lori la Tanesco lililosababisha ajali hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: