BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ISLAMIC FOUNDATION YATOA MSAADA WA VYAKULA TANI 9.3 NA NGUO KWA WAHANGA WA MAFURIKO TARAFA YA MAGOLE KILOSA MOROGORO

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akipokea sehemu ya chakula kutoka kwa Mwenyekiti wa Maafa kutoka Taasisi ya Islamic Foundation Morogoro, Ahmed Bawaziri baada ya taasisi hiyo kutoa msaada wa vifaa aina mbalimbali ikiwemo nguo na vyakula kwa ajili ya wahanga waliokumbwa na mafuriko kijiji cha Magole wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Elias Tarimo. PHOTO/MTANDA BLOG

 
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Maafa kutoka Taasisi ya Islamic Foundation Morogoro, Ahmed Bawaziri kushoto na Mbunge wa jimbo la Kilosa Mustafa Mkulo wakati wa tukio la utoaji msaada huo.PHOTO/MTANDA BLOG
Bendera akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa afya Steven Kebwe kushoto na kulia ni Mwenyekiti wa Maafa kutoka Taasisi ya Islamic Foundation Morogoro, Ahmed Bawaziri. PHOTO/MTANDA BLOG
Bendera akitoa shukurani baada ya taasisi ya Islamic Foundation baada ya Mwenyekiti wa Maafa kutoka Taasisi ya Islamic Foundation Morogoro, Ahmed Bawaziri kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya vyakula na nguo. PHOTO/MTANDA BLOG
Mwenyekiti wa Maafa kutoka Taasisi ya Islamic Foundation Morogoro, Ahmed Bawaziri akitaja vifaa vikiwemo nguo na vyakula muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada huo. PHOTO/MTANDA BLOG
Wananchi waliokumbwa na mafuriko kijiji cha Magole wakisubiri msaada katika shule ya sekondari ya kata ya Magole wilaya ya Kilosa Morogoro.
 
Na MTANDA BLOG, MOROGORO.
TAASISI ya Kiislam ya Islamic Foundation Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vyakula tani 9.3 na nguo vyenye thamani ya sh11.5milioni kwa ajili ya wahanga waliokumbwa na mafuriko katika tarafa ya Magolewi wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Maafa Taasisi ya Islamic Foundation Tanzania, Ahmed Bawaziri mbele ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera katika kijiji cha Magole alisema kuwa taasisi hiyo imetoa kiasi hicho cha chakula na nguo kwa ajili ya wahanga waliokumbwa na mafuriko katika tarafa ya Magole vyenye thamani ya sh11.5milioni na kuwa huo ni mwanza kwani bado wataendelea kutoa msaada kulingana na mahitaji ya wahanga hao.

Bawaziri alisema kuwa fedha zilizotumika kununua vifaa na bidhaa hizo zimetokana na wafadhili mbalimbali, wadau wa taasisi hiyo na wasikilizaji wa kituo cha redio Imani na watazamaji wa kituo cha televisheni cha IMAN TV ambao wamechanga fedha baada ya kutangaziwa juu ya mahitaji.

Alitaja msaada uliotolewa kuwa ni pamoja na unga wa sembe mifuko 350 sawa na tani 6.5 ikiwa na thamani ya sh6.8milioni, maharage tani 2.5 sh4milioni, mchele kilo 350 sawa na sh720,000 na nguo za akinamama, watoto, wanaume na vijana vyote vikiwa na thamani ya sh11,520,000 milioni.

Naye Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Steven Kebwe ameagiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro kufanya haraka tathimini katika vijiji vilivyokumbwa na mafuriko ikiwemo ujengaji wa vyoo katika kambi ya wahanga hao eneo la shule ya sekondari ya kata ya Magole.

Kebwa alisema kuwa lengo la kupata tathimini ya wahanga hao ni kujua idadi yao ili serikali iwe na takwimu za waathirika wa mafuriko hayo na kusaidia wadau wakuu wa serikali kuwapa takwimu ili msaada wao utolewa kulingana na idadi kamili ikiwemo idadi ya watu waliokumbwa na mafuriko katika kaya.

“Natoa agizo kwako Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Morogoro uhakikishe mpaka saa 6 usiku (wa kuamkile leo) uwe na takwimu sahihi ya wahanga wote walioathirika niwe nimeipata kwani kuna wadau wakuu wa serikali wanahitaji kupata takwimu hizo ili msaada wao watakaotoa uendane na idadi kamili ya kaya za wahanga hao”. Alisema Kebwe.

Kebwe aliongeza kuwa eneo lililotengwa kwa ajili ya mahema ya wahanga hao ambao ni wale ambao wamepoteza kila kitu ikiwemo kubomoka nyumba zao, kupotelewa vyombo vya ndani na chakula ndiyo watapewa kipaumbele katika mahitaji hayo kisha wengine watafuata.

“Hawa wenzetu waliopoteza kila kitu na mafuriko haya ndiyo wataaangaliwa zaidi kisha wengine watafuata na hapa naagiza tena ni lazima kujengwe vyoo kwa wananchi wataoishi katika mahema nah ii itasaidia kuepukana na magonjwa ya milipuko hivyo ni muhimu jambo hili kufanyika haraka”. Aliongeza Kebwe.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera alishukuru taasisi ya Islamic Foundation kwa msaada huo na kueleza waendelee kutasaidia wahanga hao kwa kila hali na mali hasa katika kipindi hiki chenye mahitaji ya kila aina.

Bendera alisema kuwa maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo ni pamoja na Magole, Mbigili, Msowelo, Makwambe, Berega, Kiegea na Dumila ambavyo kwa sasa tayari huduma za kijamii zimeanza kufanyika ikiwemo kujenga mahema, kuchimba vyoo, kusambaza majisafi na salama.

Vijiji hivyo vilikumbwa na mafuriko januari 22 mwaka huu huku baadhi yao wakipoteza mali mbalimbali ikiwemo chakula, vyombo vya ndani, mifugo na mashamba kuharibiwa na maji ya mafuriko hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: