Pikipiki ikiwa imekanyangwa na basi ndogo (Coastal) barabara ya Korogwe baada ya kutokea ajali eneo la Sido majira ya saa 1 usiku hata hivyo mwendesha pikipiki alifanikiwa kuruka na kuiacha pikipiki hiyo ikigonjwa Manispaa ya Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG
Kazi ni kazi ilimradi watoto waende chooni:Wabeba mizigo katika soko kuu la mkoa wa Morogoro wakiwa wanashusha boksi lenye samaki aina ya nguruka likiwa na ujazo zaidi ya kilo 7,00 kutoka mkoani Kigoma kwenye gari kwa ujira wa sh5,500 wakati wakifanya kazi ya kusomba kwenda katika ghala jirani na soko hilo, ambapo wabeba mizigo hao walisema wafanyabiashara wamekuwa wakiwapunja na kuomba kuongezewa pesa hadi kufikia sh10,000 kulingana na ujazo wa maboksi hayo. PHOTO/MTANDA BLOG
Jengo la shirika la nssf likiwa katika hatua za ujenzi wake linalojengwa na Group Six International ya jijini Dar es Salaam kando ya barabara ya Dar es Salaam mkabala na ofisi za halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG
Mfanyabiashara wa kuuza mkaa akiwa na baiskeli iliyosheheni magunia madogo ya bidhaa hiyo katika kitongoji cha Lukondo kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka wakati akielekea katika mji mdogo wa Mikese kwa ajili ya kusaka wateja wake mkoani Morogoro. PHOTO/MTANDA BLOG
Ombaomba akiomba wasamalia wema pesa za kujikimu na matumizi huku akiwa na mtoto mdogo ambaye hata hivyo haikuweza kufahamika kama ni mwanafunzi ama laa mtaa wa Jamattin Manispaa ya Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG
Mkazzi wa Manispaa ya Morogoro akitembeza tambi za jiko la mafuta ya taa mtaa wa John Mahenge wakati akisaka wateja wa kuwauzia mkoani Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment