BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UCHAGUZI MKUU WA NCCR-MAGEUZI WAJAA MIZENGE, JAMES MBATIA ACHAGULIWA TENA KUSHIKA NAFASI YA UENYEKITI.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, ulioitishwa ili kuwapata manaibu makatibu wakuu wa bara na visiwani na Katibu Mkuu.Kulia ni Mjumbe wa mkutano huo, Samweli Ruhuza.Picha na Silvan Kiwale.



DAR ES SALAAM.

UCHAGUZI Mkuu wa nane wa Chama cha NCCR-Mageuzi, umemchagua tena James Mbatia kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo huku mizengwe ikitawala katika uchaguzi huo.


Katika uchaguzi huo ulioanza juzi, idadi kubwa ya wajumbe walikuwa na mkakati wa kumng’oa Katibu Mkuu, Samwel Ruhuza aliyekuwa akitetea nafasi yake, Mosena Nyambabe na Rehema Sam waliokuwa wakiitaka nafasi hiyo.


Wajumbe walikuwa na mpango huo kwa kuwa Nyambabe yuko vizuri kiutendaji ikilinganisha Ruhuza. Jana kwa nyakati tofauti, wajumbe walionekana katika makundi kujadili hali hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mbatia.


Ukiacha hali hiyo, Mbatia alipata upinzani mkali akichuana kwa mbali na aliyekuwa Kamishna wa chama hicho Mkoa wa Katavi, Charles Makofila, ambaye ni mlemavu wa viungo.


Tangu kuanza kwa mkutano huo katika Ukumbi wa Diomond Jubileee, hapakuwa na dalili za upinzani wa nafasi hiyo ya uenyekiti na baadhi wa wajumbe wa mkutano walisikika wakisema, “Makofila bwana sijui amekosa cha kufanya, ila ndo hivyo wacha amsindikize mwenzake.”


Zoezi la upigaji kura lilianza saa 10 jioni hadi saa moja usiku chini ya Msimamizi wa Uchaguzi huo, Moses Machalli.


Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 228 kati ya 289.


Machalli akitangaza matokeo hayo alisema, Mbatia ameshinda kwa kura 201 na Makofila ameambulia kura 26 na kura moja imeharibika.


“Ndugu Mbatia atakiongoza chama hiki kuanza hii leo (jana) hadi Januari 2019 hivyo tumuunge mkono na uchaguzi usiwe chanzo cha migogoro, tumemaliza salama na sasa tunaangalia mbele,” alisema Machalli.


Mbatia akitoa shukrani zake alisema, “Nawashukuru sana kwa kutumia demokrasia yenu kunichagua, nawaahidi kuwatumikia kwa moyo wangu wote, uchaguzi umekwisha sasa tujenge chama chetu.”


Mwenyekiti huyo mpya, aliwataka wabunge wa chama hicho kuacha kubweteka katika majimbo yao na sasa wazunguke nchi nzima kukijenga chama.


“Machali, Kafulila kumbukeni kulipa fadhila za chama, zungukeni nchi nzima acheni kujisahau bila NCCR tusingekuwa katika Bunge tukufu, sasa kazi kwenu kwani tunaweza kama tutaamua,” alisema Mbatia.MWANANCHI









Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: