Joyce Banda alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika
April 2012. Akawa rais wa Malawi alipomrithi mtangulizi wake aliyefariki
kutokana na mshtuko wa moyo.
Michelle Bachelet amechaguliwa kama Rais wa Chile kwa muhula wa pili na kumshinda mpinzani wake Evelyn Matthei kwa kura nyingi.
Rais wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa
washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Alichaguliwa kama Rais wa
kwanza mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya
kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia.
Sheikh Hasina alichaguliwa kwma waziri mkuu wa kwanza wa Bangladesh kwa
muhula wa pili mwezi Januari mwaka 2009. Lakini mwaka 2008 chama chake
cha Awami, kilipata ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake Begum Khaleda
Zia.Korea Kusini imemchagua rais wake wa kwanza mwanamke Park Geun-hye,
kwenye uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali Disemba mwaka 2012. Babake
Park Chung-hee alitawala nchi hiyo kwa miaka 18.Waziri mkuu wa Thailand, ingluck Shinawatra dadake mdogo waziri mkuu
aliyeondolewa mamlakani Thaksin Shinawatra, aliongoza chama chake cha
upinzani kuweza kushinda uchaguzi uliofanyika Julai 2011.Helle Thorning-Schmid alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke
wa Denmark, baada ya chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi
uliofanyika Septemba mwaka 2011. Thorming alikosolewa hivi karibuni kwa
kujipiga picha na waziri mkuu wa Uingereza Cameron na Rais Barack Obama
kwenye ibada maalum ya hayati Mandela.Dalia Grybauskaite alichaguliwa kama rais wa kwanza wa Lithuania katika uchaguzi mkuu wa Mei 2009. Alishinda kwa kura 69%.
Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel anajulikana kama kiongozi asiyekuwa
na mbwe mbwe nyingi na kusababisha watu kumuita..Mutti..mama wa taifa.
Markel anajiandaa kwa muhula wa tatu baada ya kushinda uchaguzi wa
Septemba 22.Rais wa Argentina, Cristina Fernandez alishinda uchaguzi uliofanyika
mwezi Oktoba mwaka 2007 ushindi ambao wengi walisema ulitokana na
umaarufu wa mumewe aliyekuwa Rais Nestor Kirchner. Rais wa Brazil Dilma Rousseff alichaguliwa kama rais wa kwanza mwanamke
nchini Brazil alipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa Luiz Inacio Lula
da Silva mwaka 2011. Alikuwa mkuu wa majeshi kabla ya kuteuliwa na
kumrithi Rais De Silva.Kiongozi wa upinzani nchini Jamaica, Portia Simpson-Miller alishinda
uchaguzi uliofanyika Disemba mwaka 2011 kwa idadi kubwa ya kura. Alikuwa
waziri mkuu wa Jamaica kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.
Kamla Persad-Bissessar alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke
wa Trinidad and Tobago, wakati chama chake kilishinda uchaguzi kwa
idadi kubwa ya kura mwezi Mei mwaka 2010. CHANZO BBC.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / WAJUE BAADHI YA WANAWAKE AMBAO WAKO KATIKA MAMLAKA YA DUNIA KATIKA NCHI ZAO, NI VIONGOZI WANAOTIFUA KIVUMBI DUNIANI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment