Johnmarkey John
- 27 minutes ago via mobile · Like
- Annie Nyaki jaman23 minutes ago via mobile · Like
- Ibrahim Nassor Ni kwelu?5 minutes ago via mobile · Like
Mdogo wa waziri Dr Mgimwa Bw Joachim Mgimwa
WAKATI kukiwa na uvumi mbali mbali juu ya afya ya waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa(pichani) ambaye amelazwa nchini Afrika kusini kwa matibabu kwa zaidi ya wiki mbili sasa,familia ya waziri huyo imekanusha taarifa kifo cha waziri huyo na kuwa ni mzima wa afya na anaendelea kupatiwa matibabu.
Mdogo wa waziri Dr Mgimwa Bw Joachim Mgimwa ambae yupo nchini Afrika ya Kusini akimuuguza kaka yake ,alisema kuwa amekuwa akipokea simu kutoka kwa watanzania kutoa maeneo mbali mbali wakitaka kujua juu ya taarifa ambazo zimesambazwa na mitandao ya kijamii kuwa waziri huyo amefariki dunia.
Bw Mgimwa alisema kaka yake ni mzima wa afya na kwa mujibu wa madaktari wanaomtibu anaendelea vizuri na kuwa si kweli hata kidogo kama amefariki dunia.
" Ni kweli mheshimiwa waziri wa fedha na mbunge wa jimbo la Kalenga anaumwa na anaendelea na matibabu hapa Afrika ya kusini ....ukweli kwa sasa anaendelea vizuri na ninawaomba watanzania na wananchi wa jimbo la Kalenga kuondoa hofu ...mbunge wenu ni mzima kama kutakuwa na habari tofauti tutawaambia pia tunashukuru vyombo vya habari kwa kufuatilia suala hili"
Taarifa za kifo cha waziri Dr Mgimwa zilivuma pande mbali mbali za Tanzania jana
jumapili kiasi cha kuzua hali ya taharuki kwa wakazi wa mkoa wa Iringa na jimbo la Kalenga .
Miongoni mwa viongozi walioonyesha kuguswa kwa uvumi huo ni pamoja na katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa Bw Jimson Mhagama ambae hadi majira ya saa 3 usiku wa kuamkia jana alikuwa akifuatilia maeneo mbali mbali ili kupata ukweli wa uvumi huo .
" Hata mimi nimesikia kuwa waziri Dr Mgimwa amefariki dunia ila toka majira ya saa 12 jioni jumapili nilikuwa nikipiga simu huku na kule ili kujua ukweli lakini hadi sasa saa 3 hii usiku nimebaini si kweli kwani waziri na mbunge wetu ni mzima wa afya njema"
Mwandishi wa habari hizi pia alipata kuwasiliana na naibu waziri wa maji Dr Binilith Mahenge ambae alikuwa njiani kuelekea jimboni kwake Makete pia alidai hana taarifa yoyote juu ya kifo cha waziri mwenzake huyo.
Dr Mahenge alisema anatambua kuwa waziri huyo anaumwa ila hana taarifa yoyote ya kifo chake zaidi ya taarifa ya kuumwa kwake na kuwa kama angekuwa amekufa basi ingefahamika .
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Bw Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa jimbo la Ismani alisema kuwa amepata kuwasiliana na familia yake kupata ukweli juu ya uvumi huo ila hakuha ukweli wowote na kuwa waziri Dr Mgimwa ni mzima na anaendelea na matibabu.
Mtandao huu wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com unawaonya wale wote wanaoeneza uvumi wa kifo cha mpendwa wetu kuacha mara moja kwani ni kinyume na mipango ya Mungu pia tunawaomba watanzania kwa wakati huu ambao waziri wetu yupo katika matibabu kuendelea na jitihada za kumwombea afya njema ili arejee salama nchini kwa kuendelea na jitihada zake za kulitumikia Taifa na wana kalenga .
Mungu wetu wa upendo wanao tunakuomba umpe afya njema waziri wetu mpendwa.
Imechotwa: Mzee wa Matukio Blog
0 comments:
Post a Comment