WATU 10 WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO HUKU WENGINE 28 WAKIWA KATIKA HALI MBAYA NI BAADA YA BASI KUPATA AJALI MKOANI LINDI LEO.
Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo wakiwa mtaroni.. Kwakweli inasikitisha sana, hiyo ikiwa ni ajali mbaya kutokea kwa januari 20 baada ya ajali nyingine mbili ikiwemo ya Noah iliyoua watu na ile ya Mbeya kugongana magari manne kwa wakati mmoja mji mdogo wa Mbalali.
LEO majira ya saa nane alasiri Basi lenye maarufu kama ALLHAMDULILAH lilipata ajali mbaya huko mkoani Lindi watu kumi walipoteza maisha papohapo na 28 mahututi wapo Hosptali ya mkoa wa lindi sokoine,
Chanzo cha ajali hilo ni baada ya Basi hilo kugongana na
lori la mizigo wakati basi hilo likitokea Dar kuelekea Mtwara ma kupoteza mwelekeo na kupinduka mita kadhaa kutoka barabarani hali iliyochanganya na utelezi mkali kutokana na mvua kubwa iliyonjesha muda mchache kabla ya ajali.
MWENYEZI MUNGU AWATANGULIE MAJERUHI WAPONE MAPEMA, WALIOPOTEZA MAISHA MUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI.
0 comments:
Post a Comment