BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA YAANZA KWA SPEED LIGI KUU YA VODACOM MZUNGUKO WA PILI, YAILAZA ASHANTI BAO 2-1 HUKU AZAM IKIENDELEZA UBABE KWA MTIBWA SUGAR JIJINI DAR ES SALAAM.


Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi akiokoa hatari kwenye lango lake, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa jana.Yanga ilishinda 2-1. Picha na Michael 
MABINGWA watetezi Ligi Kuu, Yanga na Azam, Mbeya City wameendeleza mbio zao kileleni mwa ligi baada ya kushinda mechi zao za jana dhidi ya Ashanti United, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.


 
Yanga waliamka katika kipindi cha pili na kuichapa Ashanti kwa mabao 2-1, magoli yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na David Luhende huku Bright Obinna akifunga bao pekee kwa wenyeji.


Kwa ushindi huo Yanga wamendelea kuongoza ligi kwa pointi 31, wakifutiwa na Azam na Mbeya City zenye pointi 30, baada ya kuzifunga Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kwa bao 1-0.


Kocha wa Yanga, Hans Vans Pluijm alisema ilikuwa mechi ngumu na wapinzani wake walicheza vizuri.


“Pamoja na kushinda hatukucheza vizuri, ladha inatokana na hali ya hewa wachezaji walipata tabu kuhema.


“Uturuki kulikuwa joto nyuzi sita au 17, huku joto kali, walishindwa kucheza kitimu ni jambo nitakalolifanyia kazi. Nimefurahi kwa kupata ushindi huu.”


Yanga waliuanza mchezo wao taratibu na kuiruhusu Ashanti United kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo hali iliyofanya mashabiki wake kutoamini kilichokuwa kinatokea.


Kocha Mdachi, alilazimika kumtoa Said Bahanuzi na kumwingiza Simon Msuva dakika 35 kipindi cha kwanza mabadiliko yaliyozaa matunda kwani dakika 51, Yanga ilipata bao la kuongoza kupitia Kavumbagu aliyemalizia vizuri pasi ya Msuva.


Dakika tisa baadaye Ashanti walisawazisha bao hilo kupitia Obinna aliyemalizia kwa ufundi krosi ya Hussen Sued aliyekimbia na mpira kutoka winga ya kushoto na kupiga krosi kwa mfungaji.

Luhende alihakikishia Yanga pointi tatu muhimu dakika 79, baada ya kuwatoka mabeki wa Ashanti kwa kasi na kupiga shuti la pembeni lililomshinda kipa wa Daud Mwasongwe na kuingia wavuni.


Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni alisema amekubali matokeo, lakini wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi walizopata kipindi cha kwanza huku akimshutumu mwamuzi Abdallah Hashimu kwa kushindwa kumudu mchezo huo.


Chamazi, wenyeni Azam waliutumia vizuri uwanja wao Azam Complex na kufanikiwa kushinda kwa bao 1-0, kupitia Kipre Tchetche aliyeunganisha vizuri kazi ya Joseph Kamwaga.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: