BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BARABARA YA NDADA-MASASI HAIPITIKI NI KUTOKANA NA MVUA KUNYESHA NA KUSABABISHA MAGARI KUKWAMA MKOANI MTWARA.



Magari yakipishana kwa shida katika eneo hilo la Kijiji cha Mkalapa, Mkoani Mtwara kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo.



Wakazi wa kijiji hicho pamoja na Abiria wanaosafiri kwenda Newala, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Tunduru wakiwa wamesimama bila kujua cha kufanya wakati magari yakiwa yamekwama.



Na Abdulaziz ,Masasi.
Barabara ya Ndanda kwenda Masasi eneo la Kijiji cha Mkalapa,limekuwa ni majanga matupu kama inavyoonekana katika picha hapo chini,kwani barabara hiyo imeharibika vibara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha matika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Abiria wanaofanya safari katika maeneo hayo,inapaswa wajiandae kwa kupoteza masaa kadhaa katika eneo hilo,kwani mambo hayajakaa sawa.

Hivyo wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara (TANROADS), wanapaswa kulishughulikia swala hili haraka iwezekanavyo ili kuwaepusha watumiaji wa barabara hiyo kuondokana na hadha hii inayowaathiri wasafiri waendao Newala, Masasi, Nachingwea, Nanyumbu na Tunduru.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: