WARAKA WA MARUPU KWA
MH.RAIS JAKAYA KIKWETE NA WATANZANIA.
Natumia fursa hii kuwasilisha waraka wangu kwa Mh
Rais wa Jamhuri Ya Muungano Mh Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na mchakato mzima
wa kuwapata wawakilishi wa Bunge la Katiba.
Natumia fursa hii kuwapongeza wajumbe wote
walioteuliwa na Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXEDOxyair-bkUq_EmX0w_MV8C-XXJf4RNI6OAmsgNdKGB0p0y1XA8NGC7ZgiErSXv2rkaLUvUcqYR8zGWifXVwQt_kkUZ_9lrzV_KR5YZElOAebWozkfidY_wUC8PdFKYkCfg__ChOc4/s1600/1381392_667910669893509_1506018036_n.jpg](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXEDOxyair-bkUq_EmX0w_MV8C-XXJf4RNI6OAmsgNdKGB0p0y1XA8NGC7ZgiErSXv2rkaLUvUcqYR8zGWifXVwQt_kkUZ_9lrzV_KR5YZElOAebWozkfidY_wUC8PdFKYkCfg__ChOc4/s1600/1381392_667910669893509_1506018036_n.jpg)
RAIS KIKWETE.
Lakini nitoe pongezi zangu za dhati kwa Jukwaa la
Katiba kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuwaunganisha pamoja wana AZAKI kwa ajili
ya kufanya mchakato wa kuwapata wawakilishi wa AZAKI nchi nzima katika uchaguzi
uliofanywa siku ya tarehe 30/12/2013
Dodoma.Lakini pia tunawashukuru The Foundation For Civil Society kwa kazi kubwa kufadhili
mkutano wa kupata wawakilishi katika Bunge la katiba pitia AZAKI
Natumia fursa hii kuwataka Watanzania kuwa na imani
kubwa na wajumbe wote walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
tuwape ushirikiano wa hali na mali ili kuijenga nchi yetu ya Tanzania. Tunatoa
wito kwa wajumbe wote wanaowakilisha Asasi za Kiraia kujua mambo ya msingi
yafuatayo:-
(a)
Utaifa haujengwi na idadi ya serikali
ila unajengwa kwa uimara wa serikali. Hivyo ni jambo la muhimu sana na
kutafakari kwa kina ni muundo upi ni sahihi kwa ustawi wa Tanzania ya kesho.
(b)
Matatizo na kero zote za muundo wa serikali
wabunge wajadili kwa maslahi ya kesho. Tunaweza pata katiba mpya leo baada ya
muda wananchi wakadai katiba nyingine tena.
Na nakuunga
mkono sana Mheshimiwa Rais kwa kulisisitiza suala la mjadala wa rasimu kuwa
wa hoja. Changes are not development but
development are changes(Wilson chuchill).Katiba mpya si muungano tu tunamambo
mengi sana ya msingi ya kujadili sio muungano tu.
(c)
Natumia fursa hii kuliweka wazi suala
linaloibuliwa na baadhi ya Watanzania wenzetu wasioutakia wema undugu wetu wa
kitaifa kuhusu kudai 14km kutoka usawa wa bahari kuelekea nchi kavu kuwa ni
eneo la Zanzibar kwa mujibu wa mkataba wa Sultan Seid Said na serikali ya
Muingereza mwaka 1849.
Mkataba ule
ni aibu kuutamka kwa maana ulikuwa na vifungu 14 kifungu namba 4 cha
mkataba huo kinasema “Zanzibar will be Slave Centre for life” kwa mujibu wa
kifungu hiki sina cha kuongeza hata kidogo juu ya suala hilo. Lakini pia
mkataba wa Sultan na Uingereza hauwahusu watanzania hata kidogo kwa maana
mkataba ule ulifanyika Oman. Kitu kingine wakati mkataba unasainiwa Tanganyika
haikuwa koloni la waingereza.Sisi ni wamoja na ndugu wa kweli tusitenganishwe
na utashi.
Lakini nataka nitoe wito kwa Wabunge vijana
uliowateuwa katika Bunge la Katiba
watambue kuwa wana dhamana kubwa kuliko thamani na heshma walionayo kwa sasa.
Vijana wanaohitimu ngazi ya cheti hadi uzamivu ni milioni moja na lakini mbili
1,200,000 kwa mwaka kwa mwaka wa masomo 2012-2013.Wakati mwaka 1961 wahitimu
walikuwa 14 tu.Lakini wanaopata ajira rasmi ni vijana laki mbili tu 200,000 tu
Ni mafanikio
makubwa sana yaliyopatikana Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kazi yake imeishia hapo nyinyi kama vijana mliomo
katika Bunge la katiba mnatambua nyie ndio mtakaounda katiba itakayopelekea
mabadiliko ya sheria na sera za ajira.
Tunatoa wito kwa vijana wote kuthamini maisha ya
vijana wenzenu mliowaacha na elimu zao za cheti na shahada hawajui wataanzia
wapi huku wakisubiri wapate uzoefu wa miaka mitano (5) ili waajiriwe.
Lakini
pia muundo wa kijiografia Mh Rais ni muhimu Bunge liutazame kwa mapana sana
mfanano visiwa tulivyonavyo Tanzania havitendewi haki hata kidogo Mfano mzuri
ni kisiwa cha ukerewe chenye ukubwa wa wastani wa 6640 kirometa za mraba kina
visiwa 14 vinavyokaliwa na watu wasiopungua elfu ishirini kila kisisiwa.
Kisiwa
kama hiki kubaki kuwa wilaya hatuwatendei haki hata kidogo sambamba na kisiwa
cha Mafya ambao huduma za kimkoa zinapatikana kabaha Pwani ni mateso makali
wanayoyapata Watanzania hawa.
Mh Rais katika mabadiliko ya katiba lazima yazingatie
uiano wa kijiografia sambamba na
mahitaji ya kweli ya Watanzania.Pia sera ya Wazee waliostaafu kuangalia maslahi
yao ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zao zinazokidhi mahitaji yao ya msingi
kwa kila mwezi badala ya kulipwa kila
baada ya miezi mitatu.
Mabadiliko ya katiba lazima yasadifu stahili hizi za
watumishi waadilifu wastaafu
Natoa wito kwa wajumbe ambao hawakupata bahati ya
kuchaguliwa wasikate tamaa safari ya mafanikio haianzi kwa mafanikio.Mjitahidi
kuwajibika ipasavyo katika majukumu yetu na mafanikio yatapatikana.
Pia vijana
mnapaswa kuhakikisha mnajitokeza kujiandikisha katika daftari la kujiandikisha
kupiga kura na mnagombea nafasi mbalimbali kuanzia vitongoji na mitaa/kijiji
wakati utakapo wadia kwa mujibu wa maelekezo yatakavyotolewa na tume huru ya
uchaguzi.
Zindukeni mbadili maisha yenu sasa. Huu ndio wakati wenu vijana kutoa
maisha yenu kwa ajili ya taifa letu nguvu kazi yenu ndio msingi wa Tanzania
mpya maisha yetu hayawezi kubadilishwa bila kuzinduka, kujitoa na kuwajibika kwa
ajili ya nchi yetu amka kijana zinduka pambana tuushinde umasikini na
ujinga.
Tusijisifu kwa familia zetu kuwa
maskini tuupige vita umaskini.Na tusiendelee kuwategemea wastaafu (retired
officers) kuendelea kutuongoza sisi kama vijana tuamke sasa tuseme.
Mwisho
mh.Rais nakutakia afya njema katika ujenzi wa taifa letu huru Tanzania
karibu sana UNGO Morogoro.
Nawashukuru wana morogoro kwa ushirikiano wenu
mlioutoa wakati wote katika mchakato wa kupata wawakilishi katika bunge la
katiba asanteni sana nawashukuruni sana.Naomba kuwasilisha waraka
WARAKA HUU UMETOLEWA NA
Maliki s. Marupu
Mwenyekiti wa
Mtandao wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Morogoro (UNGO).
0 comments:
Post a Comment